BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UJENZI KWENYE BOMBA LA MAFUTA LA TAZAMA MSAMVU LAWAPONZA VIGOGO WATATU MOROGORO.


Jengo la ghorofa sita la Hoteli ya Flomi lililopo eneo la Msamvu mkoani Morogoro. Picha na Juma Mtanda.

By Hamida Shariff, Mwananchi

Morogoro. Katibu Mkuu Tamisemi, Jumanne Sagini ametoa siku 14 kwa maofisa watatu wa Manispaa ya Morogoro kujieleza ili wasifukuzwe kazi kwa kuruhusu ujenzi kwenye eneo la bomba la mafuta la Tanzania-Zambia (Tazama).

Jengo hilo la ghorofa nane la hoteli ya Flomi limejengwa kwenye eneo hatari linapopita bomba hilo katika eneo la Msamvu mjini hapa.

Amri hiyo ya Sagini imekuja kutokana na watendaji hao, Ofisa Ardhi, Ndawile Lusekelo, Mhandisi wa Majengo, Ndelebi Sengija na Ofisa Mipango Miji Steven Balonzi kudaiwa kutumia vibaya mamlaka kuruhusu ujenzi huo.

Sagini alisema maofisa hao wamekuwa wakilalamikiwa kwa kushindwa kuzuia ujenzi holela katika maeneo yasiyo rasmi, kufanyakazi chini ya kiwango na kukiuka maadili ya utumishi wa umma.

Katibu mkuu huyo alifanya ziara ya kushtukiza katika Manispaa ya Morogoro, kujionea changamoto zinazowakabili wananchi na kukagua utendaji wa kazi wa watumishi wa umma.

Akijibu maswali ya katibu mkuu, Balonzi alisema yeye ni mgeni amehamia Morogoro siku za karibuni na aliwahi kuhoji uhalali wa ujenzi wa hoteli hiyo na kuwa kwenye mchakato wa kufuatilia.

“Wakati ghorofa hili linaanza kujengwa mimi nilikuwa sijahamia hapa, hata hivyo nilipohamia tu nilianza kufuatilia kujua ni kwa namna gani ghorofa hili lijengwe mahali hapa,” alisema Balonzi.

Klabu za usiku kubanwa
Katika hatua nyingine, Sagini ametoa siku saba kwa ofisa utamaduni na ofisa biashara kuzichukulia hatua klabu za usiku ambazo hazina vizuizi vya sauti na zinazopiga muziki na kuwakera wananchi. Alisema hadi kufikia Desemba 9, kero hiyo iwe imetatuliwa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: