BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BALOZI JUMA MAPACHU AMTIMULIA VUMBI EDWARD LOWASSA BAADA YA KUSHINDWA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 25 MWAKA JANA.


Balozi Juma Mwapachu akikabidhiwa kadi ya ccm ofisi ya ccm kata ya Mikocheni leo baada ya kuamua kurejea

Dar es salaam. Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Juma Mwapachu ametangaza kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) miezi mitano tangu akihame na kuunga mkono upinzani.

Balozi Mwapachu ametangaza uamuzi huo wa kurudi kwenye chama chake cha awali leo Mikocheni jijini Dar es Salaam nakusema kuwa uamuzi huo utokana na kazi nzuri ya Rais John Magufuli.

Mwanasiasa huyo ambaye amekuwa ndani ya CCM kwa miaka 48 kabla ya kutangaza kuhama mwezi Oktoba mwaka jana na kuunga mkono upinzani, alisema kuwa chama hicho kikongwe kimepoteza dira baada ya kumnyima Waziri Mkuu mustaafu, Edward Lowassa kugombea urais kupitia chama hicho.

Balozi Mwapachu amesema kuwa baada ya miezi miwili ya uongozi wa rais Magufuli, amejiona alikosea kufanya uamuzi wa kuhama chama hicho. 


“Baada ya miezi miwili ya uongozi wa Magufuli nataka niseme nilikosea sana… Leo natangaza kurudi CCM kwasababu nimeona kazi nzuri ya Magufuli… 

Nimefanya kosa kubwa katika siasa ambalo nawasihi vijana kwenye siasa wasifanye’’ amesema Balozi Mwapachu.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: