JESHI LA POLISI LAKAMATWA MAKAHABA 500 KATIKA OPERESHENI JIJINI DAR ES SALAAM.
Wasichana wapatao 500 wanaodaiwa kufanya biashara ya ukahaba nchini Tanzania pamoja na wateja wao zaidi ya 200 wanashikiliwa na polisi nchini.
Walikamatwa kufuatia msako unaoendelea kukomesha biashara hiyo ambayo haikubaliki kwa mujibu wa sheria nchini humo.
Hii ni idadi kubwa kuwahi kukamatwa katika vita dhidi ya biashara ya ukahaba nchini humo.
Wengi walikamatwa maeneo ya Kinondoni, Temeke na Ilala 51.
Kamishna wa polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam amesema wengi wa majambazi hukimbilia kwa biashara ya ukahaba.
“Kuwakamata na kuwahoji kunasaidia kupata mambo mengi sana kuhusiana na haya (uhalifu), hata madawa ya kulevya pia. Wengi unakuta wanajua watu wanaoyatumia, wengine wanashiriki,” aliambia wanahabari.
Aliwaomba wananchi kuwasiadia maafisa wa polisi katika operesheni hiyo.
0 comments:
Post a Comment