MWANAMKE AMUITA MUMEWE TEMBO KUTOKANA NA UNENE ULIOSAABABISHA JOGOO KUSHINDWA KUPANDA MTUNGI,
Mahakama katika mji mkuu wa India imeamua kwamba ni kosa kwa mke kumuita mumewe “ndovu” na kosa hilo linaweza kuwa msingi wa talaka.
Mahakama Kuu mjini Delhi imedumisha uamuzi wa mahakama ya chini uliotolewa mwaka 2012 ambao uliidhinisha talaka.
Mahakama hiyo ilisema mtu kumuita mumewe ndovu ni “kumtendea ukatili wa kiakili”.
Mfanyabiashara aliyeitwa ndovu ana umri wa miaka 35 na alikuwa na uzani wa kilo 100.
Alisema mkewe alizoea kumuaibisha kwa kuwa mnene na "kutoweza kutimiza haja yake ya kimapenzi”, vyombo vya habari India vimeripoti.
"Hatua ya aliyekata rufaa kumbandika majina na kumrushia matusi mumewe kwa mfano kumuita 'Hathi' [ndovu], 'Mota Hathi' [ndovu mnene], hata kama alikuwa mnene bila shaka ingeathiri hadhi yake na kujiamini kwake,” Jaji Vipin Sanghi alinukuliwa na gazeti la India Today.
Mwanamke huyo alikuwa ameambia mahakama hiyo kwamba madai ya mumewe hayakuwa na msingi lakini mahakama haikukubaliana naye.BBC
0 comments:
Post a Comment