RAIS AWAPA SIKU 15 KUFAGIA WAFANYAKAZI HEWA.
Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Edward Maganga, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndg. Paul Christian Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Ikulu jijini Dar es salaam Marchi 15,2016. (PICHA ZOTE NA IKULU)
NA K-VISMEDIA/Khalfan Said
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Jumanne Machi 15, 2016 amewaapisha wakuu wa mikoa aliowateua Jumapili Machi 13, 2015 na kuwapa siku 15 kuanzia leo kuhakikisha wanasafisha wafanyakazi hewa kwenye mikoa yao na kuwaondoa kwenye orodha ya malipo ya mishahara ya kila mwezi.
Rais alisema, uchunguzi wake umebaini kuwa katika halmashauri zote nchini kuna idadi ya wafanyakazi wanaofikia 500,000(Laki tano) lakini kati ya hao wapo wafanyakazi zaidi ya 2597 ambao ni wafanyakazi hewa wanakula mishahara ya bure.
Alisema kutokana na hujuma hiyo, kwa mfano kila mfanyakazi akipokea shilingi milioni 1 ambapo wapo wengine wanapokea zaidi ya fedha hizo, basi taifa linapoteza kiasi cha shilingi bilioni 2.3 kila mwezi.
Baada yamaelezo hayo Rais amesema, nawapa siku 15 kuanzia leo muwasimamie wakurugenzi wote wa Halmashauri na kuhakikisha “wafanyakazi” hao wanaokula bila kutokwa jasho wanaondolewa kwenye orodha ya maplipo, vinginevyo ucghunguzi ukibaini basi siku hiyo hiyo mkurugenzi “atakwenda na maji” na kufikishwa mahakamni.
Rais pia amewaapisha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisiya Kuzuia na Kubapamna na Rushwa (TAKUKURU) na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), aliowathibitisha siku hiyo hiyo yaJumapili.
Katika maelekezo yake kwa wakuu hao wa mikoa, Rais amesema, wahakikishe wanapitia orodha ya watumishi kwnye mikoayao na kuwaondoa wale wote ambao hawahitajiki.
Sio kawaida ya Rais kutoa hotuba kabla ya kuwaapisha wakuu wa mikoa kama ilivyozoeleka, lakini safari hii RaisMagufuli, alianza kwa kuwahutubia huku akisoma kwenye kikaratasi hotuba hiyo ya maelekezo nakisha kuwaapisha.
Walioanza kuapishwa ni wakuu wote wa mikoa 26 ya Tanzania bara na kufuatiwa na Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata kisha
MkurugenziMkuu wa TAKUKURU Valentino Mlowola.
Meja Jenerali Mstaafu, Salum Mustafa Kijuu, Mkuu wa mkoa wa Kagera
Dkt. Rehema Jonathan Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Njombe
Ndg. Aggrey Deaisile Joshua Mwanri kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Ndg. Daudi Felix Ntibenda, Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Ndg. Amina Juma Masenza, Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Ndg.Joel Nkaya Bendera, Mkuu wa Mkoa wa Manyara
Mhandisi Mathew John Mtigumwe, Mkuu wa Mkoa wa Singida
Ndg. Jordan Mugirage Rugimbana, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Ndg. Magesa Stanslaus Mulongo, Mkuu wa Mkoa wa Mara
Ndg. Amos Gabriel Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Mhandisi Evarist Welle Ndikilo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Ndg. Said Meck Sadiki, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjalo
Ndg. Said Said Thabit Mwambungu, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Ndg. Anne Kilango Malecela, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Dkt. Kebwe Stephen Kebwe, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Zelote Steven Zelote, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Ndg. Halima Omary Dendego, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara
Ndg. Godfrey Weston Zambi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi
Ndg. Martine Reuben Shigela, Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyanga, Mkuu wa Mkoa wa Geita
Ndg. Anthony John Mtaka, Mkuu wa mkoa wa Simiyu
Meja jenerali Mstaafu Raphael Mugoya Muhunga, Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndg. Alphayo Japani Kidata kuwa kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam Marchi 15,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishina wa Polisi Valentino Mlowa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ TASWIRA YA KUAPISHWA KWA WAKUU WAPYA WA MIKOA CHINI YA UTAWALA WA RAIS DKT MAGUFULI IKULU DAR ES SALAAM
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment