Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Muhingo Rweyumamu akizungumza jambo na waumini wakati wa ibada ya pasaka iliyofanyika kitaifa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Bungo Manispaa ya Morogoro, nyuma yake ni Askofu wa Kanisa hilo la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Morogoro, Jacob Ole Mameo.PICHA ZOTE NA MTANDA BLOG
Waumini wa dini ya kikristo wakiwa katika ibada ya sikukuu ya pasaka na mbunge wa Viti maalumu Chadema mkoa wa Morogoro, Devotha Minja (wa pili kutoka kulia) katika ibada iliyofanyika kitaifa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Bungo Manispaa ya Morogoro.
Mkazi wa Kilakala, Felista Peter (30) akikabidhiwa mtoto mchanga na nesi, Patricia Nasson katika wodi ya wazazi ya 7B ya hospitali ya rufaa baada ya kujifungua katika mkesha wa sikukuu ya pasaka mkoani Morogoro, jumla ya watoto watano wamezaliwa katika mkesha huo huku watoto wa kike wakiwa wanne na kiume mmoja.
Askofu
wa jimbo la Morogoro, Telesphory Mkude akiwaosha miguu waumini wa dini
ya kikristo wakati ibada ya alhamisi kabla ya kuadhimisha sikukuu ya
pasaka inayoadhimisha na wakristo duniani kote iliyofanyika kwenye
kanisa katoliko la St Patrick mkoa wa Morogoro.
Padri
wa kanisa katoliki St Patrck katika jimbo kuu la Morogoro, Proches
Kasongo akiwa ameshikilia msalaba huku muumini wa dini ya kikristo Peter
Kimath akibusu sanamu ya yesu kikristo wakati wa ibada ya ijumaa kuu
iliyofanyika kwenye kanisa la St Patrick mkoani Morogoro.
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment