Sumbawanga. Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, imemuhukumu kifungo cha miezi sita jela Mwenyekiti wa Kijiji cha Simbwesa, Mabula Gilede (30), kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi daktari wa zahanati ya kijiji hicho, Dk Lazaro Michael.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Odila Amwol baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na kumtia hatiani mshtakiwa huyo.
Awali Mwendesha Mashtaka, Kulwa Kusekwa alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Agosti 19, mwaka jana katika Zahanati ya Simbwesa baada ya kumtuhumu daktari huyo kuwa alikuwa akitoa matibabu kwa wagonjwa kwa upendeleo.
Alidai siku ya tukio, mshtakiwa huyo alikwenda kwenye zahanati hiyo na kumshambulia kwa kumpiga kwa mateke na ngumi mganga huyo kwa madai anawatibu wafuasi wa CCM na kuwaacha wa Chadema.
Kusekwa aliendeela kudai kabla ya tukio hilo, mshtakiwa huyo alidai kuwa daktari huyo alikataa kumtibu mtoto wa rafiki yake aitwaye Milembe Machime ambaye ni mfuasi wa Chadema.
Hata hivyo, katika utetezi wake, mshtakiwa huyo aliyekuwa akitetewa na Wakili Patrick Mwakyusa alidai kuwa hakumpiga daktari huyo kama inavyodaiwa.
Alidai daktari huyo ndiye aliyempiga hadi kumuangusha chini kwa sababu alimuuliza kwanini alikataa kumtibu mtoto wa rafiki yake huyo.
Hakimu Odira kabla ya kusoma hukumu, aliiambia Mahakama kuwa kutokana na mwenendo mzima wa kesi hiyo na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka, Mahakama imemwona mshtakiwa ana hatia.
Katika utetezi uliotolewa na mwanasheria wa Gilede, Patrick Mwakyusa, aliiomba Mahakama impunguzie adhabu kwani mshtakiwa huyo ana wake watatu na watoto, pia mama yake mzazi anamtegemea.MWANANCHI
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ MWENYEKITI WA KIJIJI AFUNGWA MIEZI SITA JELA KWA KUMTEMBEZEA KIPIGO DAKTARI.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment