Yamkini bi Bule aliumwa na nyoka yapata dakika 45 zilizotangulia katika ''shoo yake'' iliyokuwa magharibi mwa Java Indonesia.
Vyombo vya habari vinaripoti kuwa muimbaji huyo nyota alimkanyaga kimakosa nyoka huyo ambaye alikuwa sehemu ya ''shoo'' yake na kwa bahati mbaya nyoka huyo akamuuma kwenye paja.
Duru zinasema kuwa alipewa dawa ya kutuliza makali ya sumu lakini akakataa akidhania kuwa nyoka yule hakumdhuru.
Aliendelea na onyesho hilo akiwatumbuiza mashabiki wake hadi pale alipoanza kutapika jukwani ndipo washirika wake wakang'amua hali haikuwa nzuri.
Mara akaanza kutetemeka na kuzirai.
Walipomkimbiza hospitalini daktari aliwaambia kuwa alikuwa ameshakata roho yake.BBC
0 comments:
Post a Comment