BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBEYA CITY FC WAPANGA MIKAKATI YA KUIMALIZA NDANDA FC PANZIA LA LIGI KUU TANZANIA 2015/16 SOKOINE MBEYA

Kikosi cha klabu ya Mbeya City FC.

KIKOSI cha Mbeya City Fc kesho jumapili kinashuka kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa kucheza mchezo wa kufungia msimu wa 2015/16 katika ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya wageni Ndanda Fc kutoka mkoani Mtwara.


Akizungumza na MTANDA BLOG, Meneja wa kikosi cha Mbeya City, Geoffrey Katepa alisema wachezaji wote 18 wametayarishwa kwa ajaili ya kuwakilisha timu yao katika mchezo huo na wako kwenye hari nzuri kutoa upinzani mkali na kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

Katepa alisema kuwa vijana wake wamemaliza mazoezi mepesi kueleka mchezo wa kesho na kila mmoja yuko vizuri na ana ari kubwa, jambo muhimu kwao ni kuona wanashinda mchezo huo ili kumaliza ligi kwa heshima na hawana wasiwasi wowote ili kumaliza msimu kwa ushindi utaowaweka kwenye mapumziko mazuri kwa matayarisho ya msimu mpya.

"City itakosa huduma ya nahodha na mlinzi shupavu wa kushoto Hassan Mwasapili aliye majeruhi kufuatia maaumivu ya nyama za paja yanayomkabili, pia Temi Felix na Deo Julius hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho kupisha majeraha waliyonayo".alisema Katepa.

Kwa upande wa mkuu wa kitengo cha utabibu Dr Joshua kaseko, ameeleza kuwa klabu itawakosa wachezaji hao kutokana na majereha waliyonayo na hiyo ina maana kuwa wataonekana uwanjani wakati wa matayarisho ya msimu mpya.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: