BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NG'OMBE KUWAPONZA WAKUU WA MIKOA MITATU ENDAPO WATASHINDWA KUTEKELEZA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS TANZANIA



Arusha
. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameagiza wakuu wa mikoa ya Geita, Arusha na Kagera kuhakikisha wanaondoa mifugo inayoingia ndani ya hifadhi ikitokea nje ya nchi na wananchi waliovamia maeneo ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) ifikapo Juni 30.

Pia, aliagiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha wanatenga maeneo maalumu kwa ajili ya mifugo inayotolewa ndani ya hifadhi, ili kupunguza migogoro.

Samia alitoa kauli hiyo jana jijini Arusha alipokabidhi hundi yenye thamani ya Sh1 bilioni kwa wakuu wa mikoa 19, ambao mikoa yao inazunguka hifadhi za Tanapa.

Alisema iwapo wakuu wa mikoa hiyo watazembea zoezi hilo, Serikali itachukua hatua za kuwawajibisha.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan
 


Alisema waliohifadhi mifugo ndani ya hifadhi hiyo waondoke na mifugo yao ifikapo Juni 30 na kwamba, Mkoa wa Kagera una ng’ombe milioni mbuili wanaotaka nje ya nchi, huku Arusha na Geita ina ng’ombe milioni tatu wa aina hiyo.

“Hatutaki kuona mifugo ya nje ya nchi ikiingia katika hifadhi zetu, nawaagiza waondoeni ng’ombe hao na mkuu wa mkoa yeyote atakayeshindwa kusimamia hili ataondoka mwenyewe,” aliagiza Samia.

Kuhusu kukabidhi hundi za ununuzi wa madawati 16,500 kwa wilaya 55 zilizopo mikoa 19, Samia alipongeza Tanapa kwa kusaidia elimu.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alisema Tanapa wanatambua mchango wa elimu ndiyo maana wametoa msaada wa madawati.

Mkurugenzi wa Tanapa, Allan Kijazi alisema wataendelea kushirikiana na serikali katika sekta ya elimu.

Akitoa shukurani, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Saidi Meck Sadiki alisema tayari mkoa huo umepiga marufuku usafirishaji wanyamapori kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) kuanzia jana.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: