BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UVUNAJI WA MKAA WAZIDI KUPUKUTISHA MITI ASILI KATIKA MISITU YA KILA KONA YA TANZANIA


MKAA.

KASI ya uvunaji wa mkaa kwa matumizi ya kibinadamu imeendelea kuathiri mazingira katika maeneo mbalimbali nchini jambo linalotishia kutoweka miti ya asili iliyodumu kwa muda mrefu na kuwapo kwa athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kutokana na hali hiyo, Shirikika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania TFCG na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (Mjumita) wameiangazia athari hiyo wilayani Kilosa na kuwashauri wadau mbalimbaku kushiriki kukabiliana na vitendo hivyo vya uvunaji ovyo wa misitu.

Akizungumza na wadau wa misitu Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro uliolenga kujadili kuhusu mpango wa uvunaji mkaa na mbao wilayani humo, na kuowashirikisha madiwani na wadau mbalimbali, Mkurugenzi wa Mjumita, Hidaya Njaidi, alikiri hali siyo nzuri kwa sababu hekta 350,000/= wilayani Kilosa pekee zimekuwa zikiteketea kila mwaka kutokana na shughuli za uharibifu wa mazingira.

Alisema shughuli hizo ni pamoja na ukataji miti ovyo, uchomaji wa misitu kwa ajili ya mkaa pamoja na upasuaji wa mbao, hali inayosababisha misitu mingi kuharibiwa na hata kutokea kwa mabadiliko ya tabianchi.

Aliwashauri wananchi na wadau wengine wa misitu wilayani Kilosa kuacha kuharibu misitu kiholela ili kuyalinda mazingira na kuikoa nchi kuzama katika janga la ukame.

Njaidi pia, aliwataka wananchi kubuni shughuli nyingine mbadala za kujiingizia kipato mbali na uchomaji wa mkaa, kwani kupitia TFC na Mjumita wamekuwa wakisaidia shughuli nyngine ikiwamo za uwindaji na ufugaji wa nyuki, nia ikiwa kuwawezesha wananchi kujimudu kimaisha badala ya kutegemea jambo moja.

Meneja Mradi wa Mkaa Endelevu (TTCS), Charles Leonard, alisema ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, ni vyema jami ikatumia njia sahihi ikiwamo waliyoanzisha kupitia mradi wa TTCS kupata mkaa endelevu, kwa kuwa njia hiyo ni salamà na inalenga kuokoa misitu na kuwafanya wananchi kuweza kujiajiri, kusaidia ulipaji wa ushuru na kukusanya mapato.

Afisa mwingine wa Mjumita, Elida Fundi alibainisha mradi huo wa uvunaji wa mkaa endelevu unalenga kuboresha namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuboresha uendelevu wa mazingira na kuongeza faida zitokanazo na rasilimali za misitu, hivyo kuleta maendeleo endelevu kwa Tanzania na wananchi wake.

Aidha, alisema mradi ulilenga pia, kusaidia wanavijiji na wadau wengine wanaotegemea sekta ya mkaa kuanzisha, kusimamia na kufaidika kibiashara kutokana na mkaa uliovunwa kiuhalali na kwa njia sahihi. 


Wadau wa misitu wilayani Kilosa wakiwamo madiwani Mariam Naheka na Ramadhani Mfaume walikiri hatari iliyopo iwapo jitihada za makusudi hazitachukuliwa kudhibiti uvunaji holela wa misitu na kupongeza jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali kubuni namna bora ya kudhibiti hali hiyo, na kwamba kupitia mradi wa mkaa endelevu, wanaamini ni fursa kwa wananchi bila kubagua jinsia katika kuongeza kipato.NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: