BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

AFYA ZA WACHEZAJI 10 WA TIMU YA SOKA YA MUHEZA UNITED FC WALIOKUMBWA NA KIPINDUPINDU ZAIMARIKA MORO.

Mshambuliaji wa timu ya Stend Misuna FC ya Singida, Steven Nzoga akimtoka mlinzi wa timu ya Mbuga FC ya Mtwara, Mohamed Fundi kulia wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa wa mikoa kituo cha Morogoro ambapo katika mchezo huo Mbuga FC ilipoteza kwa kufungwa bao 2-0.PICHA/MTANDA BLOG
Juma Mtanda, Morogoro
Afya za wachezaji 10 wa timu ya soka ya Muheza United FC zinaendelea kuimarika katika kituo cha afya Sabasaba baada ya kulazwa jana kwa kufuatia kukumbwa na ugonjwa wa kipindipindu Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na gazeti hili mjini hapa, Afisa afya wa Manispaa ya Morogoro Dkt Gabriel Malissa alisema kuwa jana (juzi) walipokea wagonjwa 11 kwa nyakati tofauti wakiugua ugonjwa wa kipindupindu na kulazwa katika kituo cha afya Sabasaba na hali zao zinaendelea kuimarika tofauti na walivyofikishwa.

Dkt Malissa alisema kuwa kati ya wagonjwa hao watatu walizidiwa lakini baada ya kupata matibabu afya zao na wengine zinaendelea vizuri.

Kwa upande wa kocha mkuu wa timu ya soka ya Muheza United FC, John King Kibwana alisema kuwa chanzo cha wachezaji hao kukumbwa na kipindupindu kumetokana na kunywa maji yasiyo salama kiafya.

Kibwana alisema kuwa jana (juzi) majira ya jioni kuanzia saa 1 hadi saa 2 usiku, kambi yao iliishiwa majisafi na majisalama na kulazimika baadhi ya wachezaji kuomba maji ya kunywa ambao waliwaelekeza kwenye kukinga maji ya bomba.

“Huu ugonjwa chanzo chake ni baadhi ya wachezaji kunywa maji yasiyo salama kiafya kwani kambi iliishiwa maji safi na salama na wakati sisi viongozi tunafanya jitihada za kupata maji safi na salama baadhi ya wachezaji walikunywa maji yasiyo salama kiafya”

Aliongeza kwa kusema kuwa wachezaji 13 na viongozi wanne wamepatiwa kinga za ugonjwa huo wa kipindupindu huku juzi jioni Iddi Ramadhan alikimbizwa baada ya kuonekana na dalili za kuhara na kutapika na kukimbizwa katika kituo cha Afya Sabasaba.

Baada ya wachezaji kunywa maji ya boma muda mfupi maji yalikatika na kuruhusiwa kunywa maji yaliyohifadhiwa katika tanki ambayo nayo yaliisha kabla ya kuteka maji ya kisima yanayohisiwa kuwaletea matatizo wachezaji hao majira ya saa 8 usiku wa juzi.alisema Kibwana.

Akiwazungumzia wachezaji ambao walizidiwa na ugonjwa huo, Kibwana aliwataja kuwa ni Iddi Bohero, Jerd Steven na Ibrahim Admin ambao hali zao zinaendelea kuimarika baada ya kupatiwa tiba pamoja na wachezaji wengine wa timu hiyo.

Kwa upande wa ushiriki wa ligi ya mabingwa wa mikoa, kocha huyo ambaye amewahi kuzichezea Coastal Union FC ya Tanga na Villa Squard ya Dar es Salaam alisema kuwa kesho (leo) timu yake itacheza na Stend Misuna ya Singida kuwania pointi tatu muhimu.

“Timu yetu ina pointi tatu baada ya kutoa sare michezo mitatu katika michezo mitatu na kesho (leo) tunacheza na timu inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi sita, hivyo tumedhamilia kushinda ili kufikisha pointi sita na kuiombea dua mbaya Namungo FC inayoongoza kwa pointi saba.”alisema Kibwana.

Kibwana alisema kuwa timu ya Muheza United FC imetua na wachezaji 23 na viongozi nne lakini kati ya wachezaji 23 wawili walikuwa wagonjwa kabla kukumbwa na kipindupindu kwa baadhi ya wachezaji.

“Bado tuna kikosi kizuri cha kupambana katika hii ligi na kupata matokeo mazuri tu kwani katika wachezaji 21 waliokuwa wazima, 10 ndio wamekumbwa na kipindupindu na kubakiwa na wachezaji 11 wazima na wale waliokuwa wagonjwa sasa hivi wako fiti kwa ajili ya mapambano.”alisema Kibwana.

Msimamizi wa kituo cha Morogoro kutoka TFF, Charles Ndagala alisema kuwa mchezo kati ya Muheza United FC na Stend FC ya Pwani uliokuwa uchezwe jana saa 8 mchana umesogezwa mbele isipokuwa kutokana na ratiba inaonyesha Muheza United FC itacheza na Stend Misuna ya Singida kesho (leo) majira ya saa 8 mchana.

Ndagala alisema kuwa mchezo huo baina ya Stend Misuna ya Singida inategemea na hali za afya na wachezaji waliopo na endapo wataonekana kuwa na matatizo leo (jana) kamati ya ligi itakaa na kuona nini cha kufanya.

Katika mchezo uliochezwa jana (juzi) baina ya Mbuga FC ya Mtwara ilishuhudia Mbuga FC ikipoteza kwa kukubali kipigo cha bao 2-0 katika mchezo uliochezwa majira ya saa 10 jioni kwenye uwanja wa jamhuri Morogoro.

Mabao ya washindi yaliyapatikana katika dakika ya 39 kwa Ibrahim Masudi kufunga bao la kwanza wakati bao la pili lilipachikwa wavuni na Hamis John.CHANZO/MTANDA BLOG
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: