Muhammad Ali alizaliwa na kupewa jina Cassius Marcellus Clay mjini Louisville, kentucky mnamo 17 Januari 1942. Alianza kucheza ndondi akiwa na umri wa miaka 12 na baadaye akaishia kushinda dhahabu katika uzani wa light-heavyweight Michezo ya Olimpiki ya Roma mwaka 1960.
Ali alianza kucheza ndondi ya kulipwa Oktoba 1960 akiwa na umri wa miaka 18 na akashinda mara 18 mfululizo kabla ya kusafiri kwenda London Juni 1963 kwa pambano lake la kwanza la kulipwa ng'ambo. Alibashiri kwamba angemshinda bingwa wa Uingereza henry Cooper kupitia knockout raundi ya tano.
Cooper alimbwaga Ali raundi ya nne lakini Mmarekani Ali alitimiza ubashiri wake kwa kumshinda raundi ya tano mbele ya watazamani 55,000 uwanja wa Wembley.
Ushindi wa Ali dhidi ya Liston ulikuwa, na bado ni, moja ya matokeo ya kushangaza zaidi katika historia ya ndondi. Ali alijisifu: "Mimi ndiye bingwa zaidi! Mimi ndiye bora zaidi! Mimi ni mfalme wa dunia!".
Ali, alitangaza kujiunga na kundi la Nation of Islam na akaacha kutumia majina yake ya awali na kuwa Muhammad Ali baada ya pambano hilo dhidi ya Liston. Alitetea ubingwa wake dhidi ya Liston mjini Lewiston, Maine mwezi mei 1965.
Novemba 1965, Ali alitetea taji lake dhidi ya bingwa wa zamani Floyd Patterson akishinda kwenye raundi ya 12. Patterson alikuwa amemshambulia sana Ali kuhusu msimamo wake kisiasa na kidini.
Ali alitetea taji lake mara ya nane dhidi ya Ernie Terell Februari 1967. Ali alimchezea Terrel ambaye alikuwa ametumia jina lake la kuzaliwa kumrejelea yeye kabla ya mechi, kwa raundi 15. Kila mara alikuwa akimwuliza: "Jina langu ni nani, Mjomba Tom?"
Baada ya kutetea taji lake tena mara nyingine dhidi ya Zora Folley, Ali alipokonywa taji lake baada ya kukataa kujiunga na jeshi la Marekani lililokuwa likipigana vita Vietnam. Ilikuwa ni miaka mitatu baadaye aliporejea ulingoni tena.
Ali alishindwa mara ya kwanza na bingwa mpya wa dunia Joe Frazier katika Madison Square Garden mwezi Machi 1971. Pambano hilo hujulikana tu kama "The Fight" yaani Pambano Lenyewe. Ilikuwa mara ya kwanza kwa mabingwa wawili wa dunia wa heavyweight ambao hawakuwa wameshindwa kukutana ulingoni.
Ali alishinda marudio ya pambano hilo dhidi ya Frazier ingawa pambano lake linalosifika sana lilijiri baadaye 1974 alipopigana na George Foreman katika pambano linalojulikana kama "Rumble in the Jungle" maana yake "Mngurumo Msituni". Ali alikaa raundi nane za kwanza akiwa amejibanza kwenye kamba, mbinu aliyoiita 'rope-a-dope'.
Ali alimshinda Mwingereza Joe Bugner mjini Kuala Limpur, malysia Juni 1975. Miezi minne baadaye, Ali alipata ushindi mwingine dhidi ya hasimu wake mkuu Frazier katika pambano la 'Thrilla in Manila'. Ali baadaye alisema lilikuwa jambo la kukaribia kifo zaidi alilowahi kuhisi.
Ali alipoteza taji lake kwa Leon Spinks 1978 kabla ya kulitwaa tena kwa mara ya tatu baadaye mwaka huo. Alitangaza kustaafu kwake miezi tisa baadaye. Lakini alirejea 1980 na kupigana na bingwa mpya Larry Holmes.Baada ya kushindwa na Holmes, Ali alipigana pambano moja, dhidi ya Trevor Berbick ambapo alishindwa kabla ya kustaafu kabisa akiwa na umri wa miaka 40. Kuondoka kwake kuliacha pengo katika tasnia ya ndondi, lililojazwa tu na kufika kwa Mike Tyson katikati mwa miaka ya 1980.
0 comments:
Post a Comment