Mwanza. Serikali imeombwa kuwachukulia hatua vijana waliowapa mimba wanafunzi na kuwasababishia kukatisha masomo yao.
Ombi hilo limetolewa leo na waathirika hao Eva Mohamed na Christina Emanuel ambao ni waathirika wa mimba shuleni wakati wa mahafali ya kuhitimu mafunzo ya kompyuta katika chuo cha Education Better for Living Organisation (Ebli).
“Serikali inapaswa kuwachukulia hatua wale wote wanaofanya vitendo hivi na kuwatelekeza wasichana,” amesema David.
Mkurugenzi wa kituo hicho, Benard Makachia alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa kituo hicho jumla ya wanafunzi 350 wamehitimu na zaidi ya asilimia 50 wamepata ajira na wengine wamepata ajira katika maeneo mbalimbali.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment