KISA CHA MAAFISA WATANO KUPIGWA RISASI KUPOTEZA MAISHA NA WENGINE SITA KUJERUHIWA VIBAYA.
Maafisa watano wa polisi mjini Dallas, Marekani wamepigwa risasi na kuuawa wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya watu weusi, Maafisa wengine sita wanauguza majeraha.
Maafisa wa polisi katika mji ulio katika jimbo la Texas, wanasema mauaji hayo yametekelezwa na washambuliaji wawili wa kulenga shabaha.
Mkuu wa polisi wa Dallas David Brown amesema amesema maafisa wa polisi bado wanakabiliana na mshukiwa mmoja ambaye anadaiwa kujibanza katika jumba linalotumiwa kuegesha magari.
“Mshukiwa huyo ambaye tunawasiliana naye amewaambia maafisa wetu kwamba mwisho unakaribia na kwamba ataumiza na kuua wenzetu wengi, akimaanisha maafisa wa usalama na kwamba kuna mabomu yaliyotegwa eneo lote, kwenye gereji na katikati mwa jiji.”
Vyombo vya habari jimbo hilo vinasema kumetokea mlipuko mkubwa eneo hilo lakini habari hizo hazijathibitishwa.
Mtu mweusi Sterling alivyouawa Marekani
7 Julai 2016 Imebadilishwa mwisho saa 13:12 GMT
Huu ndio wakati polisi walimpiga risasi na kumuua mtu mweusi Alton Sterling eneo la Baton Rouge, Louisiana. Bw Brown amesema mwanamke aliyekuwa karibu na eneo alimojificha mwanamume huyo anahojiwa na maafisa wa usalama.
atuwezi kusema kwamba tumewakamata washukiwa wote,” alisema mkuu huyo wa polisi.
Ufyatuaji risasi ulitokea mwendo wa saa tatu kasorobo usiku saa za Texas waandamanaji walipokuwa wakipitia barabara za mji na kuwafanya waandamanaji kukimbilia usalama wao.
Maandamano hayo yalitokana na kuuawa kwa wanaume wawili weusi, Philando Castile jimbo la Minnesota na Alton Sterling eneo la Baton Rouge jimbo la Louisiana.
Miongoni mwa maafisa wa polisi waliofariki ni afisa wa trafiki Brent Thompson, 43.
Raia mmoja, ambaye jamaa zake wamesema jina lake ni Shetamia Taylor, alipigwa risasi mguuni akiwakinga watoto wake na kwa sasa anapokea matibabu hospitalini.
Meya wa Dallas Mike Rawlings amesema "huu ni wakati wa kusikitisha sana kwa jiji letu.”
Rais wa Marekani Barack Obama, akirejelea takwimu zinazoonesha kwamba kuna uwezekano mkubwa wa Wamarekani Weusi kupigwa risasi na maafisa wa polisi kuliko Wamarekani Wazungu, amesema ubaguzi huo unafaa kumalizwa.
"Visa kama hivi vinapotokea, kuna sehemu kubwa ya raia wanaohisi kwamba kwa hawatendewi haki kwa sababu ya rangi ya ngozi zao, kwa sababu hawatazamwi kwa njia sawa. Na hili linauma,” amesema.
Takwimu kutoka kwa shirika linalotetea maafisa wa polisi Marekani la Officer Down Memorial zinaonesha maafisa 53 wa polisi wameuawa wakiwa kazini mwaka 2016, 21 wakiuawa kwa kupigwa risasi. Idadi hiyo haijumuishi maafisa waliouawa Dallas.
Mwanamume mmoja raia wa Uingereza anayetuhumiwa kwa kupora bunduki ya afisa mmoja wa polisi katika mkutano wa kisaiasa wa Donald Trump, amewaambia wapelelezi wa Marekani kuwa, alitaka kumuua kwa kumpiga risasi na kumuuwa mgombea huyo wa kiti cha Urais wa chama cha Republican.
Kwa mjibu wa stakabadhi za mahakama, Michael Sandford anasema kuwa aliendesha gari hadi Las Vegas akiwa na nia ya kumpiga risasi Bw Trump siku ya Jumamosi.Awali Donald Trump alimtimua Maneja wake wa kampeni Corey Lewandowski kwa kutofautana naye katika kauli zake.
Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden amemlaum Trump kwamba kauli zake ni za hatari.Chanzo BBC.
0 comments:
Post a Comment