TCRA YAILAZIMISHA CLOUDSTV KUOMBA RADHI KWA SIKU TANO BAADA YA KURUSHA KIPINDI CHA TAKE ONE KWA KUMHOJI SHOGA.
Dar es Salaam. Kituo cha televisheni cha Clouds kimetakiwa kuomba radhi kwa siku tano kupitia taarifa zake za habari kutokana na maudhui ya kipindi cha Take One kilichomuonyesha mwanaume anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Hukumu hiyo ilisomwa jana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),
Joseph Mapunda na kubainisha kuwa, Juni 28, mwaka huu, kituo hicho kilirusha kipindi hicho saa 3:00 usiku, mtangazaji Zamaradi Mketema alifanya mahojiano na kijana aliyejitambulisha kuwa ni shoga.
“Kipindi kimeonyesha wazi jinsi ushoga unavyofanyika pamoja na mbinu zinazotumika, lugha iliyotumika katika mahojiano haikuwa na staha,” amesema Mapunda.
0 comments:
Post a Comment