BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VIJANA 42,400 WA CHADEMA KUTOKA MOROGORO KWENDA DODOMA KUSAIDIANA NA POLISI KUZUIA MKUTANO WA CCM DODOMA


 

Juma Mtanda,Morogoro
Baraza la Vijana la chama cha Demokrasia na Maendeleo mkoa wa Morogoro (Bavicha) linakusudia kupeleka vijana 42,400 ili waweze kuongeza nguvu kwa upande wa jeshi la polisi katika kuwazuia ama kuwatawanya wanachama wataokaidi agizo la kutekeleza kauli ya Rais John Magufuli ya kuzuia vikao vyote na mikutano ya vyama vya siasa mpaka mwaka 2020.

Hatua hiyo ya Bavicha inakuja baada ya kuwepo kwa taarifa za chama cha Mapinduzi (CCM) kudaiwa kuwepo kwa dalili za kufanya mkutano mkuu wenye lengo la kukabidhiana madaraka ya nafasi ya mwenyekiti taifa ndani ya CCM kutoka kwa rais mstaafu, Jakaya Kikwete kwenda kwa Rais John Magufuli Julai 23 mwaka huu mkoani Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za wilaya ya Chadema mjini hapa, Mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Morogoro, Barnabas Okola alisema kuwa Bavicha wanakusudia kuwapeleka vijana 42,400 hivyo Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, David Misime kutakiwa kuwapokea kati ya Julai 21 na 23 mwaka huu katika kijiji cha Chalinze Nyama.

Okola alisema kuwa tayari wameanza maandalizi ya kuwaorodhesha vijana hao kutoka kwenye kata mbalimbali zinazounda mkoa wa Morogoro kwa wilaya zake nane ambapo kazi hiyo inafanywa na wenyeviti wakisaidiana na makatibu wa wilaya hizo.

Aliongeza kwa kusema mikutano ya Chadema imekuwa ikizuiliwa na katika kuona hilo, Chadema inataka kusaidia jeshi la polisi kuzuia mkutano ya CCM unaotarajiwa kufanyika Julai 23 kwa lengo la kubadilishana uongozi katika ya mwenyekiti wa sasa wa CCM na rais mstaafu wa awamu ya nne na Rais John Magufuli.

Kwa upande wa Mwenyekiti Bavicha wa wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro, Peter Mdidi alisema kuwa vijana wapo katika majimbo 11 ya kila kata 212 ambayo itatoa zaidi ya vijana 200 ili kuzuia mkutano huo unaoitwa kuwa ni haramu utavunja demokrasia nchini.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: