BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAGONJWA WASITISHIWA CHAKULA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MOROGORO

 
Morogoro. Baadhi ya wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro wanakabiliwa na wakati mgumu baada ya kutangaza kusitisha rasmi mgawo wa chakula uliokuwa ukifanyika kila siku kwa zaidi ya miaka 10.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hii kwa masharti ya kutotajwa majina yao, baadhi ya wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo wamesema uamuzi huo wa hospitali unawaathiri kwani fedha walizokuwa wakitumia kwa matibabu inabidi wazigawanye ili wapate chakula.

Omega John anayemuuguza ndugu yake katika wodi namba 9 amesema uamuzi huo wa hospitali umekuja ghafla na hata wagonjwa hawajapata muda wa kujiandaa kwa kuwa tangazo limetolewa siku mbili kabla ya utekelezaji.

“Chakula kimesitishwa kutolewa hapa hospitali tangu tarehe moja mwezi wa saba na tangazo limewekwa siku moja tuu kabla ya utekelezaji,” amesema John.Chanzo.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: