BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ASKARI WA JESHI LA POLISI AUAWA KWA KUCHOMWA SHINGONI


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi

ASKARI Polisi mwenye namba G.5092 PC John Nyange (28), aliyekuwa anafanya kazi katika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mwanza, ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mtu aliyekuwa na ugomvi naye.

Akizungumza na wandishi wa habari jana jijini hapa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 21, mwaka huu saa 4 usiku katika eneo la klabu maarufu iliyoko katika Manispaa ya Ilemela ya Villa Park Resort iliyopo katika kata ya Kirumba.

Alisema chanzo cha mauaji hayo ni kuwa Nyange, alikuwa na ugomvi wa muda mrefu na Magina Hussein (27) ambaye ni fundi wa kompyuta na mkazi wa mtaa wa Kigoto katika manispaa ya Ilemela.

“Nyange alikuwa anamdai Magina kompyuta mpakato yake ndipo usiku wa kuamkia jana, saa 4 usiku walikutana katika Klabu ya Villa Park ambapo mtuhumiwa wa mauaji hayo inasemekana akiwa na wenzake watano, walimvamia na kumchoma na kitu chenye ncha kali shingoni na alifariki dunia akiwa njiani wakati akipelekwa hospitali kwa matibabu,” alifafanua.

Akielezea wasifu wa marehemu, Kamanda Msangi alisema alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Stefano kilichoko mjini Moshi.

“Alikuwa anasoma shahada ya sayansi ya habari na mawasiliano mwaka wa pili, alikuwa likizo na alikuja Mwanza kuiangalia familia yake na ndipo alipokutwa na mauti,” alisema.

Alisema watu sita akiwemo Magina, ambaye alikuwa na ugomvi na Nyange na wenzake watano, wamekamatwa na wanahojiwa na Jeshi la Polisi kuhusiana tukio hilo.

“Aidha upelelezi wa tukio hili bado unaendelea na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi,” aliongeza.

Msangi alisema kuwa Polisi Mkoa wa Mwanza imesikitishwa na kifo cha askari huyo, kwani imempoteza askari kijana ambaye Jeshi la Polisi lilikuwa bado linamtegemea.

Alitoa mwito kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza kuacha tabia ya kuchukua sheria mkononi na kusababisha mauaji yasiyo ya lazima kwa kuwapiga watu wengine hadi kuwaua.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: