MANENO YA BUSARA KUTOKA KWA MWIGULE NCHEMBA ! TUSIISHIE KULAANI TU PINDI MATUKIO YA KIHALIFU YANAPOTOKEA, WANANCHI SAIDIENI KUWAFICHUA.
Jana usiku Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchinim, Mwigulu Nchemba alifika eneo la mji wa Mbande wilaya ya Temeke muda mchache baada ya kutokea tukio baya la uhalifu wa kutumia silaha ambapo watu/majambazi zaidi ya saba wakiwa na silaha wamevamia eneo la Benki ya CRDB-Mbande na kuua askari wanne.
Askari hao walishambuliwa kwa kufyatuliwa risasi wakati wakishuka kwenye gari tayari kwa kupokezana lindo.
Nchemba anaeleza kuwa pia majambazi hayo katika tukio hilo wamefanikiwa kuwajeruhi raia wa kawaida wawili na aliweza kuwajulia hali zao huku wote wakiendelea vizuri.
"Hatutaishia kulaani tu tukio hili na matukio mengine kama haya, natoa rai kwa wahusika kujisalimisha,Vilevile wananchi na raia wema tunaomba ushirikiano wenu katika vita hii ya kupambana na wahalifu hawa na wanaotuzunguka kwenye maeneo yetu."alisema Nchemba.
0 comments:
Post a Comment