Mbao Fc imefungwa bao 1-0 dhidi ya Mwadui Fc lililofungwa na Abdallah Sesemi uwanja wa CCM Kilumba jijini Mwanza, Simba Sc ilivutwa sharubu na Ruvu JKT baada ya sare tasa ya bao 0-0 uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Mtibwa Sugar ilipata ushindi wa bao 2-1 mbele ya Ndanda Fc wakai Stend Unitend ilishindwa kutamba kwa Kagera Sugar zilitoshana nguvu kwa sare ya bao 0-0 Shinyanga Kambarage, Prison na Shootinga sare ya bao 0-0 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Majimaji ilikubali kipigo cha bao 3-1 kutoka kwa Azam Fc.
Katika michezo ya kesho Yanga Sc itacheza mchezo wake wa kwanza na African Lion Fc uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku Mbeya City Fc itacheza na wenyeji wao Toto African Fc katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
0 comments:
Post a Comment