BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UBABAISHAJI WAMFANYA KATIBU WA CHADEMA MKOA WA MWANZA KUJIVUA VYEO VYOTE NA KUJIUZURU.

Aliyekuwa Katibu wa Chadema Mkoa wa Mwanza, John Nzwalile.Picha na mtandao

Mwanza.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Mwanza, John Nzwalile amejivua nyazifa zake tatu pamoja na uanachama wa chama hicho kwa madai kuwa chama hicho kimekuwa na ubabaishaji.

Mbali na ukatibu wa mkoa, Nzwalile alikuwa mjumbe wa Baraza Kuu Taifa na mjumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Mwanza, Nzwalile amesema Chadema kimekuwa kikiwachonganisha wananchi na Serikali, jambo ambalo amesema halikubaliki.

“Nimefikia uamuzi huu mgumu wa kujivua nyadhifa zangu zote na uanachama wa Chadema baada ya kuchoshwa na siasa za uchochezi, majungu na uchonganishi zinazofanywa na chama hiki kikubwa cha upinzani nchini,” amesema Nzwalile.


Aliongeza kwa kusema kuwa imefika hatua viongozi wa Chadema wakijifungia ndani kwenye vikao vyake vinahusu maandamano na uchochezi pekee, kwanini “tusifanye shughuli za maendeleo badala ya kuhamasiha vurugu na uvunjifu wa amani. amehoji Nzwalile.Mwananchi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: