BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UKAWA WAARISHA MAANDAMANO YA UKUTA KESHO TANZANIA, WASOGEZA MWEZI MMOJA MBELE

Tokeo la picha la photos of EDWARD LOWASSA
Muungano wa vyama vya upinzani nchini Tanzania umeahirisha maandamano ya kitaifa ambayo yalikuwa yamepangiwa kufanyika kesho.

Viongozi wa upinzani, akiwemo Edward Lowassa wa Chadema, wametangaza hatua hiyo kwenye kikao na wanahabari Dar es Salaam.

Wamesema wameahirisha maandamano hayo kwa kipindi cha mwezi mmoja baada ya kusikia ombi la viongozi wa kidini na wadau wengine waliowaomba kukumbatia na kuyapa muda mazungumzo.

Viongozi wa chama hicho walikuwa wameitisha maandamano na mikutano ya kisiasa Septemba Mosi kupinga walichosema kuwa ni ukandamizaji unaoendelezwa na serikali.

Baada ya mkutano wa kikao cha Kamati Kuu ya chama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwishoni mwa Julai, viongozi walisema: "Yapo Matukio ambayo yamekua yakifanywa na kukandamiza demokrasia na misingi ikipuuzwa na kudharauliwa."
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: