MVUTANO kati ya Jeshi la Polisi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ulihitimishwa jana baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kutumia dakika 28 kusoma tamko la kuahirisha maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika leo nchi nzima.
Maandamano hayo yasiyo na kikomo, yalikuwa yameandaliwa na Chadema kupitia operesheni wanayoiita Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta) iliyozinduliwa Julai 27, mwaka huu. Jeshi la Polisi mapema lilikuwa limepiga marufuku vyama vya siasa kufanya maandamano na mikutano ya hadhara katika kutekeleza amri ya Rais John Magufuli, ambaye aliagiza ya kutaka mambo hayo kusubiri Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
0 comments:
Post a Comment