BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

LIGI DARAJA LA KWANZA NETIBOLI LAFIKIA PATAMU MOROGORO

Mfungaji wa timu ya netiboli ya Polisi Morogoro GS, Mwanaidi Hassani akichuana na mlinzi wa timu ya Tumbaku ya Morogoro, Aziza Shiza GK na wengine wakati wa ligi daraja la kwanza netiboli Tanzania bara 2016/2017 katika uwanja wa jamhuri Morogoro ambapo katika mchezo huo Tumbakuwa ilifungwa vikapu 58-45.Picha na Juma Mtanda.
Juma Mtanda,Morogoro. jphtjuma@gmail.com.
Wakati timu ya netiboli ya Jiji Tanga ikijinasua kutoka mkiani katika msimamo wa ligi daraja la kwanza netiboli Tanzania bara 2016/2017 inayoelekea ukingoni, timu ya maafande wa jeshi la Polisi Morogoro yenyewe ndio inayoonekana kujitutumua na kuikaba koo bingwa mtetezi wa ligi hiyo Uhamiaji ikipigana vikumbo kugombea nafasi ya kwanza mkoani hapa.

Timu za Uhamiaji na Polisi Morogoro ndizo zenye uhakika wa kutwaa ubingwa huo baada ya kushuka dimbani mara nane na kila moja ikivuna pointi 16 huku Uhamiaji ikiizidi maarifa kidogo Polisi Morogoro katika magoli ya kufunga na kufungwa kufuatia Jeshi Star kujiondoa katika mbio hizo.

Wenyeji Polisi Morogoro katika michezo hiyo imefunga magoli 550 na kufungwa 240 wakati Uhamiaji ikiongoza ligi hiyo kutokana na kufunga magoli 661 na kufungwa magoli machache 175 dhidi ya Polisi Morogoro.

Kwa upande wa timu ya Jiji Tanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Modesret Mshata ambayo iliyokuwa ikiburuza mkia kwa muda mrefu imepata ushindi wake wa kwanza na pili na kujikusanyia pointi nne.

Jiji Tanga ilipata ahueni na kupumua na kupata ushindi baada ya kuifumua timu kibonde ya Kinondoni kwa vikapu 44-32 huku ikijitutumua na kupata ushindi mwingine wa pili kwa kuilaza timu ya Ras Kagera kwa magoli 35-26 na kuifanya kuwa na pointi nne.

Jiji Tanga ilipata ushindi huo kupitia kwa wafungaji wao tegemeo GS, Hadija Amani na Jane Daudi baada ya kurekebisha makosa yao ya upachikaji magoli katika michezo iliyotangulia baada ya kukutana na timu za Kinondoni na Ras Kagera.

Katika matokeo ya michezo mingine Jeshi Stars iliifunga Madini Arusha kwa magoli 57-40 huku Jiji Arusha ikipoteza mchezo wake mbele ya Tumbaku Morogoro kwa magoli 72-46 na Polisi Morogoro ikiilaza CMTU magoli 61-36.

Kinondoni ilikubali kipigo kutoka kwa Jiji Arusha kwa magoli 65-27 na Tumbaku Morogoro ilipoteza mchezo wake kwa Madini Arusha kwa magoli 52-39 wakati Polisi Arusha ikajikuta inatandikwa vikapu 66-37 kwa ndugu zao Polisi Morogoro na Ras Kagera ikilala kwa kupoteza mchezo na Uhamiaji wa magoli 97-15.

Timu ya Uhamiaji ilipata ushindi mwingine kwa kuilarua Polisi Arusha kwa vikapu 98-18.

Kwa upande wa Jeshi Stars yenye pointi 10 inachuana vikali kugombea nafasi ya tatu ya ligi hiyo na Madini Arusha yenye pointi tisa zote zikiwa zimebakiwa na michezo miwili mkononi.

Timu ya Polisi Arusha yenyewe imekusanya pointi sita sawa na CMTU yenye pointi sawa huku Polisi Arusha ikiwa imezidi mchezo mmoja mbele ikitofautiana vikapu vya kufungwa na kufunga.

Polisi Arusha imefunga vikapu 399 na kufungwa vikapu 450 wakati CMTU ikiwa imefunga vikapu 310 na kufungwa vikapu 288 na timu ya Kinondoni ikiwa haina pointi baada ya kupoteza michezo yake nane na kubebeshwa lundo la kapu la magoli 607 na kufunga magoli 169.Chanzo/MTANDA BLOG
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: