BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS MAGUFULI AWAIBUA WASOMI ZIARA YA KIKAZI ZANZIBAR

Rais John Magufuli.
Dar es Salaam. Kauli za Rais John Magufuli kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar zimewaibua wasomi na wanasiasa, wakimtaka akubali kuwa visiwa hivyo vina mkwamo wa kisiasa na kuhitaji majadiliano.

Akihutubia wananchi kwenye Uwanja wa Gombani ya Kale kisiwani Pemba Ijumaa iliyopita, Rais Magufuli alisema uchaguzi umekwisha na hivyo wananchi wasitarajie kama kutakuwa na jambo jingine zaidi ya kusubiri uchaguzi mwingine mwaka 2020.

Juzi Rais Magufuli, ambaye amepiga marufuku mikutano ya siasa hadi mwaka 2020, alitoa hotuba nyingine kwenye Uwanja wa Demokrasia (zamani Kibandamaiti) kwa wananchi wa Unguja iliyozungumzia uhasama wa kisiasa ulioibuka visiwani humo. 


Rais Magufuli katika hotuba yake alimshauri Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk Ali Mohamed Shein kutoidhinisha malipo ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa iliyokuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuwa alikataa kumpa mkono wa salamu walipokutana kwenye mazishi ya Rais wa zamani wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: