BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANAFUNZI WA DARASA LA SABA 795,761 KUFANYA MTIHANI WA KUHITIMU ELIMU YA MSINGI SEPTEMBA 7 NA 8 MWAKA 2016


 
Picha ya maktaba ikiwaonyesha wanafunzi wa shule ya msingi Mwere Manispaa ya Morogoro wakifanya mtihani. MTANDA BLOG.

JUMLA ya watahiniwa 795,761 wanataraji kufanya mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi nchini (PSLE) kwa mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk Charles Msonde amesema wanafunzi hao wamesajiliwa kufanya mitihani yao Septemba 7 na 8 mwaka huu.

Msonde amesema wanafunzi hao watafanya mtihani ya kiswahili, Kiingereza, Sayansi, Hisabati na Maarifa ya jamii.

Wanafunzi 763, 602 walifanya mitihani hiyo mwaka 2015 na wanafunzi 518,034 wakafaulu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: