WATU SABA HUFARIKI DUNIA KWA AJALI KILA SAA 24 TANZANIA
CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) kimetoa takwimu zinazoonyesha kuwa watu 1,580 walifariki dunia kutokana na ajali hizo katika kipindi cha miezi saba kuanzia Januari hadi Julai mwaka huu, ikiwa ni wastani wa watu saba kila siku.
Aidha Tamwa imeomba kufanyika kwa marekebisho ya sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuweka sheria ambayo itasaidia kupunguza ajali za barabarani zinazoendelea kuua watu nchini.
Katika taarifa ya chama hicho iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa, Edda Sanga, alisema mabadiliko hayo yanayopaswa kufanywa, yaiguse pia Sheria ya Usalama Barabarani ya Mwaka 1972.
0 comments:
Post a Comment