MANENO YALIYOJAA MAUMIVU YA MOYO, NI NADRA KUTAMKWA NA MGONJWA ZAIDI YA KULIA TU.
“Nimepokea majibu haya kwa majonzi nilijua siku moja nitakufa, lakini sijawahi kuhisi kama nitakuja kutobolewa macho na visu. Aliyefanya kitendo hiki amenitoa mshipa na siwezi tena kuona. Nina majonzi makubwa, lakini sina jinsi sitaweza kuona tena, tukio hili limezima ndoto zangu zote....
Naumia sana ninaposikia mama yangu anataka kunipa jicho lake moja ili nione, lakini najua leo ataumia zaidi. Nawashukuru sana hasa wewe Mkuu wangu wa Mkoa, mke wangu, ndugu zangu na ninyi waandishi wa habari, sina cha kuwalipa,” ni maneno yaliyosemwa na kijana Said Mrisho baada ya kupokea majibu ya Daktari kuwa hatoweza kuona tena.
0 comments:
Post a Comment