BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NAULI ZA BEI KWA NDEGE MPYA ZA ATCL DAR-MWANZA NI SH160,000/=



SHIRIKA la Ndege (ATCL) limetangaza nauli za ndege mpya zitakazoanza rasmi safari zake keshokutwa huku njia ya Mwanza-Dar es Salaam ikipangiwa nauli nafuu kwa lengo la kushinda ushindani uliopo kati yake na mashirika mengine.

Mbali na njia ya Mwanza-Dar, shirika hilo lililotoa ratiba ya wiki mbili mpaka Oktoba 28 litakuwa pia na ruti nyingine tatu ikiwemo visiwa vya Comoro.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Mhandisi Patrick Itule, aliiambia Nipashe juzi kwa simu kuwa ushindani katika ruti hiyo ni mkubwa kulinganishwa na maeneo mengine nchini.

Alisema nauli ya Dar-Mwanza itakua Sh. 160,000 kwenda pekee wakati kwenda na kurudi itakuwa Sh. 320,000 kwa daraja la kawaida.

Nauli hizo ni nafuu kulinganishwa na mashirika mengine yanayofanya safari za ndege nchini likiwamo shirika jingine la nauli za bei nafuu la Fastjet ambalo nauli ya Mwanza - Dar es Salaam (kwenda pekee) ilikuwa Sh. 212,000 (pamoja na VAT) Julai mwaka huu.
Mbali na ATCL na Fastjet, shirika lingine linalohudumia njia hiyo ni Precission Air.

Alisema kigezo kikubwa walichokitumia katika kupanga ruti hizo ni jinsi ya kuliepuka shirika kujiendesha kwa hasara kama ilivyokuwa awali.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, ndege hizo kwa awamu hii ya kwanza zitafanya safari za Mwanza-Dar, Dar-Arusha, Arusha-Zanzibar na Dar-Comoro.

Alisema tayari tiketi za ndege hizo zimeanza kununuliwa na kwamba tiketi za gharama kubwa kwa ndege zao zitakuwa kwa wale wanaokata za muda mrefu.

“Kuna tiketi za muda mrefu, unakuta mteja anaenda nchi fulani anakaa mwaka mzima, hizi tiketi gharama yake ni kubwa na haiwezi kulingana na ile ya miezi sita, mitatu au mwezi mmoja kama tulivyopanga," alisema. "Nauli ya Sh. 160,000 iliyopangwa ni ya wiki mbili."

Alisema nauli ya daraja la kawaida ya kutoka Mwanza-Dar kwenda pekee ni Sh. 160,000 huku ile ya kwenda na kurudi ikiwa ni Sh.320,000.


Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, nauli za ndege hizo kwa daraja la juu ‘Business Class’ kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma ni Sh. 590,000 na ile ya kwenda na kurudi ni Sh. 910,000.

Kwa ruti za Dar es Salaam kwenda Kigoma kwa wale watakaopanda daraja la kawaida ‘Economy Class’ kwenda peke yake ni Sh. 395,000 wakati ya kwenda na kurudi itakuwa ni Sh. 610,000.

Safari ya kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa daraja la biashara, nauli yake ni Sh. 478,000 wakati ile ya kwenda na kurudi ikiwa ni Sh. 735,000.

“Daraja la juu nauli ya kutoka Dar es Salaam kwenda Bukoba Sh. 520,000 na tiketi ya kwenda na kurudi itakuwa ni Sh. 800,000 na kwa daraja la kawaida kwenda peke yake ni Sh.325,000 na tiketi ya kwenda na kurudi itakuwa ni Sh. 499,000,” alisema.

Alisema nauli ya daraja la juu kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ni Sh. 478,000 kwa safari moja na kwa tiketi ya kawaida na kurudi itakuwa ni Sh. 735,000 wakati kwa daraja la kawaida kwenda peke yake itakuwa ni Sh. 325,000 na tiketi ya kwenda na kurudi ni Sh. 495,000.

Kadhalika kwa wale wanaosafiri kutoka Dar es Salaam hadi Mtwara, nauli ya kwenda kwa daraja la juu ni Sh. 450,000 na kwenda na kurudi itakuwa ni Sh. 695,000 wakati daraja la kawaida nauli ya kwenda pekee itakuwa ni Sh. 305,000 na kwenda na kurudi ni Sh. 470,000.

Aidha, safari ya kutoka Dar es Salaam hadi Mbeya kwa daraja la juu itakuwa ni Sh. 480,000 kwa ruti moja na wale watakaotaka tiketi ya kwenda na kurudi bei itakuwa ni Sh. 740,000 na kwa daraja la kawaida itakuwa ni Sh. 160,000 kwa ruti moja na kwenda na kurudi ni Sh. 320,000. 


“Daraja la juu kwa ruti moja kutoka Mwanza kwenda Bukoba ni Sh. 378,000 na kwa tiketi ya kwenda na kurudi ni Sh. 580,000 wakati ruti moja kwa daraja la kawaida itakuwa ni Sh. 140,000 na tiketi ya kwenda na kurudi kwa watakokata itakuwa ni Sh. 280,000,” alisema.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: