BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NJIA YA KUFANYA UTAFITI NA KUBAINI TABIA ZA BAADAYE ZA MTOTO


UTAFITI kuhusu kutabiri mustakabali wa baadaye tabia ya mtoto, umefanyika kwa mafanikio.

Watafiti wa sehemu mbalimbali, ikiwemo Marekani na New Zealand, wanasema majaribio ya awali yameonyesha dalili njema ya hatima ya baadaye ya mtoto katika umri wa miaka mitatu tu.

Kupitia utafiti huo unaofanyika kwa majaribio ya ubongo wa mtoto, umebaini ni rahisi kumgundua kijana hata mtoto kama ana mwelekeo wa kuwa mhalifu au mtu mwema wa tabia katika siku hizo za baadaye na mafanikio yake kwa jumla.

Miongoni mwa wanayoyafanyia kazi, ni pamoja na uwezo wa kutumia lugha, ambayo inatoa ishara ya mwelekeo wa mtoto huyo.

Ni utafiti unaodokeza hata kama mtoto hatakuwa na mwelekeo wa kuwa mhalifu, jambo linalosaidia kujenga mazingira ya kumkinga baadaye.

Kazi hiyo ilifanyika nchini New Zealand na matokeo yake kuwasiliswa katika jarida la kisayansi.

Watafiti hao kutoka Chuo Kikuu cha Duke nchini Marekani, wanasema hiyo inatoa ishara ya umuhimu wa kuwa na ufahamu sahihi kuhusiana na maisha ya baadaye ya mtoto na hatima yake, ili kufungua mlango mzuri wa mtazamo wa namna ya kuchukua hatua sahihi.

Ingawaje utafiti umefanyika kwa wakazi wa New Zealand, lakini yatokanayo yanaweza kutumika katika nchi nyingi. Ilihusisha watoto
1,000.

Namna walivyooanisha, ni kwamba walipata maksi ndogo katika somo la stadi za lugha kwa watoto hao wa miaka mitatu, iliyomaanisha wana dalili ya kuwa wahalifu katika siku za baadaye au kuwa na tabia mbaya.

Hata hivyo, utafiti huo kuhusu mustakabali wa baadaye wa mtoto haukuhusu hatima ya kiuchumi, iwapo atakuwa ama maskini au tajiri.

Wataalamu wanasema, mbali na mtazamo huo wa awali wa mtoto katika umri wa miaka mitatu, bado wana nafasi ya kubadilika sana kitabia, iwapo watasimamiwa vyema.

Wataalamu kwa muda mrefu wamekuwa wakieleza umuhimu wa watoto kupata elimu ya awali, kama njia mojawapo ya kuwarekebisha na kupata mwelekeo sahihi wa maisha ya baadaye.

Mtaalamu Prof. Terrie Moffitt, kutoka Chuo Kikuu cha Duke cha Marekani,ambaye alikuwa kiongozi mwenza katika utafiti huo anasema:"Kadri watoto wanavyosimamiwa mapema ndiyo inakuwa vizuri zaidi.

"Hii ni kwa sababu, mtoto anapelekwa kusiko sahihi katika umri wa miaka mitatu na wanaangukia katika mwelekeo usiowandaa katika maisha sahihi ya utu uzima."

Prof. Moffitt, anasema takriban watoto wote wenye maksi za chini katika vipimo vya ubongo wao wana hatari ya kuangukia pabaya.

Anasema utafiti unabashiri vijana hao wadogo wenye nafasi mbaya, ni wale waliokosa fursa muhimu na bora kwa maandalizi ya maisha yao ya baadaye.

Kwa mujibu wa profesa huyo mtafiti, jamii inaoaswa kubadilika kutoka kundi la kulaumu kwamba watoto kwamba ni ‘wapotezaji’ na badala yake kuwa nafasi ya kuwapa msaada zaidi.

Prof. Moffitt alifanya utafiti kwa kushirikiana na mume wake, Prof. Avshalom Caspi, kutoka chuo cha King's cha London, Uingereza.

Mtafiti huyo mwenza – mwanaume, anasema wana matarajio kwamba matokeo ya utafiti huo yatazishawishi serikali duniani kuwekeza katika usimamizi wa awali wa maisha ya watoto.

"Nitarajia kwamba, kilichofanywa na utafiti wety si udhanifu,” anasema Prof. Caspi na kuongeza:

"Ninatarajia kwamba utafiti wetu utajenga utashi wa umma na msukumo wa kisiasa kuingilia kati masuala ya watoto na familia, ili wapate mwanzo mzuri wa maisha yao.

ELIMU YA AWALI
Kwa mujibu wa Josh Hillman, Mkurugenzi wa Taasisi ya Nuffield Foundation, anasema wameshatambua umuhimu wa elimu ya awali.

"Hata hivyo, utafiti huo mpya unapendekeza kuwa, wasipuuze hata kidogo umuhimu wake," anasema.

Hivi sasa msisitizo unaoelekezwa nchini Uingereza ni kwamba,kuwepo elimu bora. Utafiti ulifanywa kwa kushirikisha wataalamu wa afya na kushirikisha watu 1,037.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: