BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TIMU YA SOKA YA VIJANA YA RICHIE ACADEMY FC YATWAA KOMBE LA U16 MOROGORO

Nahodha wa timu ya vijana ya Richie Academy ya Dar es Salaam, Seleman Augustino akiwa ameshika kombe la ubingwa wa Chuma Kifimbo Cup 2016 akishangilia na wachezaji wenzake mara baada ya kuitandika Tysco Academy bao 4-0 katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo yaliyofikia tamati jana kwenye uwanja wa Moro Youth mkoani Morogoro.

Juma Mtanda, Morogoro.
Timu ya soka ya Richie Academy FC imetwaa ubingwa wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 16 ya Chuma Kifimbo Cup 2016 baada ya kuisambaratisha Tysco Academy kwa bao 4-0 zote za Dar es Salaam katika mchezo mkali wa fainali uliopigwa kwenye uwanja wa Moro Youth mkoani hapa.

Tysco Academy ilishindwa kuhimili kasi na mikimiki ya vijana wenzao Richie Academ FC na kuruhusu mashmbulizi ya mara kwa mara katika lango lao yaliyopelekea kutandikwa bao hizo.

Mshambuliaji hatari wa Richie Academ FC wa mashindano hayo alifunga bao la kwanza kabla ya nahodha wao, Seleman Augustino kupachika bao la pili huku Shabaan Mangula na Rashid Kilongo wakishindilia kwa kufunga mengine likiwemo bao la tatu na nne katika ushindi huo mnono.

Richie Academ FC ilifika hatua hiyo ya fainali baada ya kuiadhibu AICT Adacem ya Morogoro kwa bao 3-0 katika mchezo wa hatua ya nusu fainali wakati Moro Kids ilifungashiwa virango baada ya kufungwa kwa njia ya penalti 3-2 dhidi ya Tysco Academy katika hatua hiyo ya nusu fainali.

Kutokana na kutwaa ubingwa huo, timu ya Richie Academy FC ilikabidhiwa kombe na seti moja ya jezi na mwandaaji wa mashindano hayo taasisi ya Morogoro Youth and Woman Soccer Development Centre (Moro Youth) huku Tysco Academy iliyoshika nafasi ya pili akikabidhiwa mipira miwili.

Mshindi wa tatu timu ya Moro Kids iliambulia zawadi ya mpira mmoja huku mashindano yakishirikisha jumla ya timu 16, timu nne kutoka Dar es Salaam na 12 Morogoro.

Mratibu wa mashindano hayo, Rajabu Kindagule alisema kuwa changamoto kubwa ya kuendesha mashindano hayo ni upande wa zawadi kutokana na wadau kushindwa kuyaunga mkono.

“Haya mashindano ndio chimbuko la bora la soka na kuwaendeleza vijana wetu lakini vijana wanahitaji kupata hamasa kwa kuwapa zawadi, unaweza kuona hii leo tumekosa kutoa zawadi ya mfungaji bora, mchezaji bora, kipa bora, timu yenye nidhamu na haya yote yanachangia mtoto kujituma zaidi na kuendeleza kipaji chake na chachu ya kujinza zaidi.”alisema Kindagule.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: