Juma Mtanda, Morogoro.
Tukio la mkazi wa kitongoji cha Upangwani kijiji cha Dodoma-Isanga, Augostino Mtitu (42) kuchomwa mkuki mdomoni na kutokea shingoni limechukua sura mpya baada ya chama cha wafugaji Tanzania kulaani vikali kitendo hicho huku jeshi la polisi likiwashikiria wafugaji 12 kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo
Tukio hilo lilitokea Desemba 25 mwaka huu majira ya saa 5 asubuhi mkoani Morogoro.
Tukio hilo lilitokea kata ya Masanze wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro kwa wakulima tisa kujeruhiwa vibaya katika ugomvi huo unaodaaiwa kuzuka baada ya wafugaji kudaiwa kuingiza mifugo kwenye shamba lenye mazao.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za chama cha waandishi wa habari mkoani hapa, Naibu Katibu Mkuu wa chama cha wafugaji Tanzania, Joshua Lugaso alisema kuwa chama chao kinalaani kitendo cha, Augostino Mtitu kuchomwa mkuki mdomoni na kutaka serikali kumchukua hatua kali za kisheria mtuhumiwa endapo atabainika na makosa.
Lugaso alieleza kuwa chama hicho kimesikitishwa na kustushwa kwa tukio lililotokea la, Agustino Mtitu kuchomwa mkuki mdomoni katika mzozo kati yake na wafugaji wa kabila la Wamasai na kumsababishia maumivu makali baada ya kujeruhiwa.
“Umoja wetu umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya tukio hilo na tunalaani vikali kitendo hiki kilichofanywa na wafugaji hao na zaidi ya yote umoja wetu hauungi mkono vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria na haki za kibinaadamu na kujichukulia sheria mkononi”.alisema Lugaso.
Aliongeza kwa kusema kuwa wanatoa pole kwa Mtitu na familia yake na kumuombea dua njema ili apone haraka jeraha aliyoyapata lakini pia sheria itachukua mkondo wake kwa wote waliohusika katika tukio hili.alisema Lugaso.
Lugaso alieleza kuwa katika migogoro ya ardhi baina ya wafugaji na wakulima yapo matukio yanayopelekea jamii hizo kupoteza maisha hivyo ni jukumu la pamoja kukemea na isiangaliwe jamii moja pindi inapotokea imefanya mabaya ndio ikemewe.
“Kuna matukio mengi ya wafugaji nao kupoteza maisha katika migogoro hii ndani ya Tanzania hivyo jamii isisubiri wafugaji wamefanya tukio ndio kuwe na sauti kubwa nafikiri jamii hizi zinategemeana na hakuna kiongozi wa mfugaji au mkulima anaweza kuunga mkono vurugu zinazopelekea mtu kupoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu.”alisema Lugaso.
Kwa mujibu wa Naibu Katibu mkuu huyo, alieleza kuwa chanzo kikubwa cha mgogoro huo ni watu kujichukulia sheria mikononi kwa wakulima kukusanyika na kudhuru mifugo iliyongia shambani kwa kuikata na mapanga na ng'ombe 13 kujeruhiwa vibaya katika tukio hilo.
“Ikifuata sheria pande zote mbili na kuheshimi mipaka yao, ukatili dhidi ya mifugo na ukatili dhidi wa wakulia itakuwa njia sahihi ya misingi ya amani, umoja na upendo ndio watanzania kitu tunachonivunia.”alisema Lugaso.
Lugaso alieleza kuwa wana imani na serikali ya awamu ya tano lakini iweke mkazo katika kuinua zaidi sekta ya mifugo ili iweze kuchangia zaidi pato la taifa ambapo kwa sasa inachangia kwa 7% pekee.
“Serikali ikithamini mchango wa wafugaji itenge maeneo toshelevu na yenye miundo mbinu kwa kilimo na ufugaji ili kutenganisha kilimo na ufugaji na kukufanya hivyo kutazuia migogoro hii ya mara kwa mara”alisema Lugaso.
Moja ya sababu zinazodaiwa kuchochea migogoro ya wafugaji na wakulima ni viongozi wa serikali na kisiasa kuingilia migogoro hiyo upande mmoja huku jamii nyingine ikitengwa.
Endapo kamati za maridhiano zitaundwa na kuzipa nguvu zitasaidia kupata suluhu ya kweli ya kujengea roho ya upendo na undugu lakini serikalo inaweza kudhibiti utungwaji wa kiholela wa sheria kandamizi dhidi ya Wafugaji zinatungwa katika halmashauri za vijiji. Alisema Lugano.
Moja ya mifano ni pale ng'ombe anapokamatwa baada ya kuingia shambani, hutozwa kiasi cha sh200,000 ambapo faini hiyo ni sawa na kuuziwa upya ng’ombe huyo hivyo inapaswa kuangaliwa upya.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema kuwa wafugaji hao wanashikiliwa kwa tuhuma za kuwashambulia kwa silaha za jadi na kuwajeruhi watu sita wakazi wa kitongoji cha Upangwani kijiji cha Dodoma Isanga wilayani Kilosa.
Alisema kuwa kujeruhiwa kwa wananchi hao kulitokana na kitendo cha wananchi kukamata mifugo ya mfugahi Ngayoni Kiming'ati iliyokuwa ikiharibu mazao yao ya mahindi na watu saba wamefikishwa mahakamani huku wengine uchunguzi ukiendelea.
Kamanda Matei alitoa onya kwa wafugaji kuacha kuwatumia watoto kuchunga mifugo na kutembea na silaha kama mikuki na sime wanapokwenda kuchunga mifugo yao huku akiwataka wakulima nao kuacha tabia ya kujeruhi mifugo kwani inachochoa migogoro.
0 comments:
Post a Comment