BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

AFRIKA YA KUSINI NA CHINA ZASHINDANA VIKALI KUWAFUNGA JELA WATANZANIA KWA MAKOSA YA MADAWA YA KULEVYA.



Mtanzania Pamela Kirita (41) na Thelma Mkandawire (38) raia wa Zambia baada ya kukamatwa kwa tuhuma madawa ya kulevya. 

JUMLA ya Watanzania 578 wamekamatwa na kufungwa katika magereza ya nchi mbalimbali kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Akiahirisha mkutano wa sita wa Bunge la 11 mjini Dodoma juzi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alitaja nchi ambazo Watanzania hao wamefungwa kuwa ni pamoja na China (200), Brazil (12), Iran (63), Ethiopia (7) na Afrika ya Kusini (296).

Majaliwa pia alisema vita inayoendelea nchini dhidi ya dawa za kulevya inapaswa kuungwa mkono. Alisema madawa ya kulevya huingia zaidi kutumia kwa njia za bandari bubu kupitia Bahari ya Hindi na mipakani kwa njia ya magari binafsi na mabasi yatokayo Kenya, Uganda na Zambia.

“Lengo la serikali ni kuwasaidia walioathirika na dawa za kulevya na kuwachukulia hatua kali wale waliowaathiri - wauzaji na wasambazaji," alisema Majaliwa.

"Dhamira ya serikali ni kupambana na janga hili kwa dhahiri na kwa dhati bila kumuonea mtu yeyote na kwa kuzingatia misingi ya sheria na haki.”

Vita dhidi ya madawa ya kulevya katika jiji la Dar es salaam inaingia wiki yake ya tatu kesho, baada ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kutaja zaidi ya watu 75 ambao wanatakiwa kuisaidia polisi kuhusiana na biashara ya mihadarati nchini.

Orodha ya makonda imejumuisha polisi, wasanii, wanasiasa na wafanyabiashara.

Na vita hiyo ilipata nguvu zaidi mwanzoni mwa wiki baada ya Rais John Magufuli kusisitiza yeyote ambaye anajihusisha na mihadarati kukamatwa bila kujali wadhifa wake kwenye jamii.

“Hakuna mtu maarufu, mwanasiasa, waziri au kiongozi yoyote au mtoto wa fulani, askari ambaye anajihusisha na dawa za kulenya aachwe, hata awe mke wangu Janeth... kamata wote weka ndani,” alisema Rais Magufuli.

Alisema biashara ya dawa za kulevya kwa sasa nchini imefikia katika hali mbaya na kwamba zinauzwa kama njugu. Alitaka vyombo vyote vya ulinzi vinavyoendelea kupambana na dawa za kulevya viendelee na mapambano.

Alisema biashara ya dawa za kulenya kwa sasa nchini inapoteza nguvu kazi za Watanzania wengi haswa vijana, na kwamba vyombo vyote vya ulinzi vinapaswa kushirikiana ili kuwakamata hao.

Rais Magufuli aliwataka wahusika kuuwinda mtandao wote unaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya. “Haiwezekani wauzaji wapo mtaani wanatanua tu, hawakamatwi," alisema Rais Magufuli.

"Kwa mfano kuna muuzaji mkubwa yupo mkoani Lindi, alishikwa na dawa za kulevya lakini sijasikia hata siku moja akitangulizwa Mahakamani. "Ninajua kuna viongozi wanamtetea.”

Rais Magufuli alikuwa akimzungumzia mtu anayeaminika kuwa 'mzungu wa unga' aliyekuwa akitafutwa zaidi nchini.

Ali Khatibu Haji (47), maarufu kwa jina la Shikuba, alikamtwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Machi, 2014 baada ya kuwindwa kwa miaka miwili kabla ya kuhamishiwa mkoani Lindi.


Anatuhumiwa kuwa kiongozi wa genge lenye makao yake Afrika Mashariki lakini likiwa na uhusiano wa kibiashara mpaka China, Brazil, Canada, Japan, Marekani na Uingereza.Nipashe
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: