MACHINGA SASA KUONDOLEWA BARABARANI KATIKA OPERESHENI MAALUMU
KAMATI ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, imeanza operesheni maalumu ya kuwaondoa machinga waliovamia hifadhi za barabara za Jiji la Mwanza.
Akithibitisha mpango huo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha alisema operesheni hiyo inalenga kuwaondoa machinga waliovamia maeneo yasiyo rasmi; hasa ya kandokando ya barabara za Nyerere, Rwagasore Pamba, Uhuru na Kenyatta.
Alisema machinga walio katika maeneo hayo wanafanya shughuli zao kinyume cha sheria na kuwataka waende maeneo ya Tanganyika, Sahara, Mtaa wa Sokoni, Makoroboi na Dampo.
Alisema anasikitika kuona suala hilo la kuwaondoa machinga wanaovunja sheria kwa kupanga bidhaa zao kila mahali linaelekea kutoungwa mkono na viongozi wa wafanyabiashara ndogondogo hao hata hivyo.
Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba amewataka maafisa watendaji wa mitaa na kata kuhamia kwenye maeneo yao ya kazi na watakaokiuka agizo hilo watachukuliwa hatua kali.
0 comments:
Post a Comment