BANGI CHANZO KIZURI TU, CHA MAGONJWA YA AKILI
Mbeya. Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya ya Rufaa Kanda ya Mbeya (MRH), amesema watu watano au sita kati ya 10 wanaougua na kupata matibabu ya ugonjwa wa akili hospitalini hapo walivurugikiwa baada ya kutumia bangi kwa wingi.
Akizungumzia madhara wanayopata watumiaji wa cocain na heroini kwa muda mrefu, Dk Lawala amesema wanaoacha kutumia hukosa usingizi na wengine huharisha mfululizo. Madhara mengine ni ugonjwa ya mapafu, moyo, ini na figo.
Pia, husababisha vifo vya ghafla hasa wanaojidunga kutokana kuzidisha dozi, kuchangia kuenea kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), kifua kikuu na virusi vya homa ya ini aina ya B na C.
Madhara mengine kuwa ni watumiaji wengi kukabiliwa na magonjwa ya meno na ngozi yakiwamo majipu, vidonda na ukurutu.
0 comments:
Post a Comment