SAMAKI ANAYEZALISHA UMEME NDANI YA MAJI NDIYE HUYU.
Na Geofrey Chambua
Duniani yapo mengi ambayo yanavuta hisia ukiyasikia. Wengi wetu huamini kuwa umeme umekuwa ukizalishwa kutoka katika vyanzo mbalimbali kama mashine, betri, jua na maji.
Lakini amini au usiamini kuna viumbe ambao wanazalisha umeme mwingi wenye nguvu hata ya kuweza kumuua binadam mtu mzima ndani ya sekunde...lakini pia hata MAMBA HAFUI DAFU kwa samaki huyu achilia binadamu
Moja ya viumbe wenye uwezo wa kuzalisha umeme ni samaki aina ya electric eel au electricus fish ambae ana umbo refu mfano wa bomba huwa akikuwa anaweza akafikia urefu wa mita 2 ( futi 6-7) na uzito wa kilo 20 kitu kinachomfanya kuwa samaki mkubwa katika kundi la Gymnotiformes.
Katika samaki anayeogopeka na kumshika kwake lazima uwe makini huyo electric fish. wanakuambia hata aikwa nje ya mtumbwi anauwezo wa kutoa umeme wa kutosha kukuumiza sentimita chache kutoka alipo....NASIKIA HAPA Tanzania pia wapo (ila sio Kamongo)
Electric eel ana viungo tofauti vinavyomsaidia kuzalisha umeme, cha kwanza kinazlisha umeme kwa ajili ya kuwindia na kingine kinazalisha kwa ajili kusikilizia.
Viungo hivi vya kuzalishia umeme vinatengeneza 4/5 ya mwili wake wote, na vinmuwezesha kuzalisha umeme wa aina mbili ule wenye nguvu kubwa na ule wa nguvu ndogo. Viungo hivi ambavyo vimeundwa na elektroliti vimejipanga kwa pamoja ambapo ngunvu ya umeme inapita kama vile ufanyavyo kwenye waya.
Kipindi eel anapohisi windo ubongo wake hutuma taarifa kwenye elektroliti na hii hupelekea kufungua chaneli ya madini yachuma ambayo inaruhusu sodium kupita kwa kubadili mkondo kurudi nyuma ambapo mabadiliko ya haraka hutokea katika mkondo na kupelekea kuzalisha umeme kama vile betri ambapo seli hupangwa pamoja ili kupata umeme. Ndani ya electric eel, baadhi ya seli 5,000 mpaka 6,000 zilizojipannga kwa pamoja ambazo zina uwezo wa kuzalisha volt 860 na watt 860 ndani ya chini ya sekunde moja. Umeme huu una uwezo wa kumdhuru hata kumuua mtu mzima.
Pia ndani ya smaki huyu kuna ogani nyingine ijulikanyo kama Sach’s ambayo inaundwa na seli nyingi ambapo kila seli inazalisha umeme mdogo wa volti 0.5, organi hii inazalisha umemewa 10V katika mawimbi ya 25hHz kwenda juu , ambapo huutumia umeme huu mdogo kwa ajili ya kufanya mawindo yake hasa ukizingatia kuwa hana macho.
Pindi samaki huyu anapojihakikishia kuwa windo lake lipo ndani ya mzio wake basi huachia ule umeme mkubwa ambapo ukimpata windo basi hupoteza nguvu na hivyo kumezwa na samaki huyu.
Electric eels amekuwa akifanyiwa uchunguzi wa bioelectrogenesis. Na amekuwa ni kivutio kwa watafiti, ambapo watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani na wizara ya taifa ya teknolojia wanajalibu kuona kama wanaweza kutengeneza seli feki zinazofanana na za samaki huyu au kuboresha seli za samaki huyu. Uzalishaji ama uboreshaji wa seli hizo unaweza kuendelezwa kisayansi ili kuweza kuwa kama chanzo cha nguvu kwa viungo vya vya bandia na vifaa tiba.
Electric eels anaishi katika maji ya baridi(yasiokuwa na chumvi) katika msitu wa Amazon na katika bonde la mtoOrinoco huko America kusini. Na maranyingi hupatikana katika kina cha mto katika maji yaliyotulia kiasi.
Chakula chake kikubwa ni wadudu, konokono, kaa, minyoo ingawa mala nyingine anaweza kula samaki na wanyama wadogo wadogo kama panya.
Uzalialianaji wake ni wa kutaga mayai kipindi cha kiangazi ambapo hutaga mayai karibia 3000. Samaki jike ndio mwenye umbo dogo kuliko dume.
0 comments:
Post a Comment