SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, ameonyesha kurudi nyuma katika nia yake ya kuwapima wabunge kilevi kabla ya kuingia ukumbini, baada ya kukumbushwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, juzi.
Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Ndugai alisema ataanza kupima wabunge kilevi pale hali ya matumizi ya vilevi itakapokuwa mbaya bungeni.
Mei 23, mwaka jana, Spika Ndugai aliieleza Nipashe kuwa kuna wabunge kadhaa huingia ukumbini wakiwa wametumia vilevi vikali vikiwamo bangi, viroba na 'unga' hivyo ana mkakati wa kuweka vifaa maalumu vya kupimia ulevi kwa wabunge wote.
Ndugai alielezea nia hiyo ikiwa ni siku chache tangu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, afukuzwe kazi na Rais John Magufuli kwa kujibu swali bungeni akiwa amelewa.
Ndugai, hata hivyo, alisema ameupokea ushauri uliotolewa juzi na Makonda kama ushauri mwingine wowote kwa mhimili huo wa dola.
Spika Ndugai alisema kwa sasa uongozi wa Bunge hauna mpango wowote wa kutekeleza zoezi hilo.
Nipashe ilizungumza na Ndugai kutaka kujua umepokeaje ushauri wa Makonda, ambaye alikuwa akimkumbusha kauli yake mwenyewe.
Aidha, Nipashe ilitaka kufahamu kama kuna hatua zozote zimeshachukuliwa tangu Mei, mwaka jana, kuweka kipimia ulevi kwa wabunge katika ukumbi wa watunga sheria hao mjini Dodoma.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi orodha mpya ya watuhumiwa 97 wa biashara haramu ya dawa za kulevya na kumkaribisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rodgers Sianga, Makonda alimkumbusha Spika Ndugai kuhusu kusudio lake hilo.
Makonda alisema utaratibu wa kuwapima wabunge kabla hawajaingia katika ukumbi wa Bunge utakuwa mzuri.
"Na utaratibu huu wa kuwapima wabunge wetu utakuwa mzuri sana, na ninakumbuka kuna kipindi Spika aliwahi kutangaza kuuanzisha, lakini sijui ukaishia wapi, nitoe tena rai kwake afikirie tena kuanzisha utaratibu huu," Makonda alisema.
"Siamini kama Spika alisema hili kwa bahati mbaya, isipokuwa alimaanisha, na kama ni hivyo asifikirie kuwapima na katika suala la dawa ili kubaini kama wanatumia au la."
Lakini Ndugai alisema kwa sasa hakuna mpango kama huo wa kuwapima wabunge ili kuwabaini wale waliotumia kilevi, lakini endapo hali ya matumizi ya dawa za kulevya ikizidi kuongezeka watalazimika kufanya hivyo.
“Kwa sasa ni mapema mno kuanza utaratibu huo, na hadi sasa hatuna mpango huo, endapo tukianza tutawataarifu” alisema Ndugai.Nipashe
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ PAUL MAKONDA AMKUMBUSHA SPIKA WA BUNGE KUWAPIMA ULEVI WABUNGE KABLA YA KUINGIA BUNGENI DODOMA
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment