CHADEMA YAPATA PIGO BAADA YA MBUNGE WAO KUFARIKI DUNIA NCHINI UINGEREZA
Mbunge wa Viti Maalum, Chadema Dk Elly Macha.
Mbunge wa Viti Maalum kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) Dk Elly Macha amefariki dunia leo nchini Uingereza ambapo taarifa ya kifo chake imetolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha bunge.
Katika taarifa hiyo imeeleza kuwa Dk Macha alifariki dunia wakati akipata matibabu katka hospitali ya New Cross, Wolverhamton iliyopo nchini humo.
Dk Macha alikuwa akiwakilisha watu wenye ulemavu bungeni kupitia chama chake cha Chadema.
Wakati huo huo bunge limeahirisha vikao vya kamati vilivyokuwa vikiendelea leo hadi hapo kesho Aprili Mosi.
0 comments:
Post a Comment