BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHAMA CHA WANASHERIA CHAJIINGIZA KWA WAPENZI WA JINSIA MOJA ZANZIBAR


CHAMA cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) kimesema mpango wa serikali wa kuwakamata watu wanaotuhumiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja lazima izingatie misingi za haki za binadamu na utawala bora visiwani hapa.
 Akizungumza mjini hapa jana, Rais wa chama hicho, Omar Said Shaban, alisema ZLS haipingi kufanyika kwa operesheni hiyo, lakini inataka ifanyike kwa umakini mkubwa ili kuepusha kuvunja haki za msingi za kikatiba ikiwamo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha kwa mujibu wa sheria.

Alisema ZSL imepokea malalamiko ya watu waliokamatwa katika kumbi za burudani na nyumba za kulala wageni na kuhusishwa na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Alisema watu hao wanalalamika haki zao za msingi za kikatiba kuvunjwa baada ya kukamatwa wakiwa katika matembezi ya kawaida na kisha kufanyiwa uchunguzi sehemu za siri na wengine kuonekana hawajawahi kushiriki vitendo hivyo.

“ZLS tunaunga mkono jitihada za kupambana na makosa ya jinai kama mapenzi ya jinsia moja, dawa za kulevya na ukahaba, lakini lazima haki za binadamu zizingatiwe katika utekelezaji wake.”

"Mtu anaweza kukamatwa palepale kama amefanya kosa la ghafla, lakini haiwezekani mtu kukamatwa bila ya kuwapo hati ya kukamatwa kwake wakati yupo katika matembezi ya kawaida au mikusanyiko halali."

“Baadhi ya waliokamatwa wamefika ofisini tumewapokea na kuwapa ushauri wa kisheria, jambo kubwa wanalalamika wamedhalilishwa kwa kukamatwa wakiwa katika kumbi za starehe na nyumba za wageni,” alisema Shaban ambaye ni Wakili wa Mahakama Kuu Zanzibar.

Akizungumzia malalamiko ya watuhumiwa hao kunyimwa huduma za kisheria na baadhi ya mawakili Zanzibar pamoja na kuwa tayari kulipia gharama, Shaaban alisema suala la wakili kupokea kesi au kukataa ni hiyari yake mwenyewe.

“Wakili ninaweza kukataa kesi kama kuna mgongano wa maslahi au mlalamikiwa ni mteja wangu au ndugu yangu, lakini tumewasikiliza kwa umakini kutafuta ukweli wake,” alisema.

Masako wa kuwatafuta watu wanaofanya mapenzi ya jinsia na wanawake wanaojiuza unaendelea kufanyika katika nyumba za kulala wageni na kumbi za starehe mjini hapa, ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. 


Mpaka sasa majalada 16 ya watu wanaotuhumiwa kufanya vitendo hivyo yamekabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP), Ibrahim Mzee, kwa ajili ya hatu zaidi za kisheria.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: