Rais Dk Mohamed Shein
akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)
Jenerali Venance S. Mabeyo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar hivi karibuni.
Na Mwinyimvua Abdi, Zanzibar.
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein anatarajia kuzindua rasmi michezo ya
majeshi Tanzania (BAMATA) ikishirikisha michezo mbalimbali kesho kenye uwanja
wa Amaan Visiwani humo.
Mkuu wa majeshi ya ulinzi Tanzania na Mwenyekiti wa Baraza la michezo ya majeshi
Tanzania (BAMATA) Jenerali Vennance Mabeyo amezungumza huku akiwataka wananchi kujitokeza
kwa wingi kushuhudia michezo hiyo.
Michezo hiyo itashirikisha vikosi vya ulinzi na usalama ambayo mashindano
hayo yaliyoanzishwa rasmi mwaka 1984 huku yakishindwa kufanyika kwa muda wa
miaka 13 kutokana na uchache wa rasilimali.
Akizungumza hivi karibuni katika mkutano na waandishi wa habari makao makuu
ya Brigedi ya Nyuki Migombani Zanzibar, alisema kuwa Rais Dk Shein ndiye
atayezindua mashindano hayo itayohusisha michezo ya soka kwa wanaume, mpira wa
pete wanawake, mpira wa mikono (hand ball), mpira wa kikapu (basket ball), na
mpira wa wavu (volley ball) kwa wanawake na wanaume.
Jenerali Mabeyo alisema kuwa wananchi wa Zanzibar ameomba wajitokeza kwa
wingi kwenye uwanja wa Amani ili kuwaongezea ari ya ushindani kwa wanamichezo ili
wafanye vizuri zaidi na kupata hali itakayoviimarisha vikosi hivyo kama
ilivyokuwa katika miaka ya nyuma kupitia michezo hiyo.
“Miaka mingi wanamichezo na timu za majeshi zimekuwa zikifanya vyema katika
michezo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa jambo lilioonekana kufifia katika
miaka ya karibuni hivyo anaamini mashindano hayo yataibua ari na mwamko wa timu
hizo kufanya vyema”.alisema Jenerali Mabeyo.
Mwenyekiti huyu alizitaja timu zitakazoshiriki kuwa ni ngome inayoundwa na
jeshi la ulinzi wa wananchi wa Tanzania (JWTZ), jeshi la kujenga taifa (JKT),
polisi, magereza, uhamiaji, zimamoto na timu ya vikosi vya idara maalum ya SMZ.
Mabeyo ambae ambae pia ni mkuu wa jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania
(JWTZ) aliyataja mashindano hayo pia kuwa ni miongoni mwa majukwaa
yanayowakutanisha wanajeshi kwa lengo la kuimarisha upendo na maelewano
miongoni mwao ndio maana bamata imeona haja ya kuyaendeleza.
“Pamoja na kushindana katika michezo mbali mbali, mwisho wa yote sote tutakuwa
washindi kwa kuwa mashindano haya yapo kwa ajili ya kuendeleza umoja na
mashirikiano yetu kama wadau katika ulinzi na maendeleo ya taifa letu”, alisema
Mkuu huyo wa majeshi.
Aidha Jenerali Mabeyo alivipongeza vyombo vya habari nchini kwa kuwa karibu na
kutangaza habari na matukio mbali mbali yanayolihusisha jeshi hilo, na kuwaomba
kufanya hivyo katika mashindano hayo ili kuwahamasisha watazamaji na washiriki
wa michezo hiyo.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment