MAMBO YA KUFAHAMU KUHUSU NCHI YA CAPE VERDE
Na Geofrey Chambua1)
Cape Verde ni kisiwa kwa muonekano kinafanana sana na Zanzibar, ingawa yenyewe ina majabali makubwa (Partly Rock City). Ni Visiwa vyenye milima ya volkano vya Cape Verde, nje ya pwani ya magharibi mwa Afrika vina mambo mengi hasa fukwe ambazo huwavutia watalii.
Ili kufika Cape verde ni lazima hutokee moja ya nchi za West Africa sana sana Senegal na nchi za jirani na Senegal kwa maana hakuna ndege za moja kwa moja mpaka Praia.
Mji mkuu wa Cape verde ni Praia na sarafu ya nchi Hiyo huitwa Escudo.
Ilikuwa na idadi ya watu laki nne na nusu tu.(nb: yaweza ongezeka) wanawake ikiwa ni laki tatu na wanaume laki na nusu........ idadi ya watalii wakati mwingine inazidi idadi ya wananchi.... Watu wa Cape verde ni machotara wa Kireno na Weusi, mfano wa wazawa wa Cape verde ni mwanamitindo maarufu wa Marekani Amber Rose. lugha kuu ni kireno Rais wao aliwaomba kila mcape verde wa kiume awe na mahusiano walau na wanawake wawili ili kufanya kila mwanamke apate mwenza. (Tushukuru hiyo nchi ipo mbali. nahisi wanaume wa Wabongo wangehamia huko)
Dunia nzima kuna wa Cape verde million mbili tu(nb: idadi yaweza kuongezeka), wa cape verde wengi wanaishi nchi za ulaya Ureno ikiongoza.
Kuna mtanzania mmoja tu tena mwenye asili ya Zanzibar anayeishi na kufanya biashara ya mgahawa nchi Cape verde. Siku za mapumziko (Wikiend) kwa wa Cape verde inaanza Jumatano mpaka Jumapili, (ni wavivu na wapenda starehe pesa zao nyingi utumwa na ndugu zao wanaoishi bara Ulaya).......Cha nyongeza, jamaa wanapenda sana kufanya jogging jioni. Ni sehemu ya maisha yao ya kila siku.
Ukiwa na mahusiano na msichana wa Kicapeverde unaweza kwenda nyumbani kwa wazazi wake na kufanya mapenzi uku wazazi wakiwepo sitting room bila kujali then ukajiondokea bila tatizo lolote wao ni kawaida tu.
Kuna wakati timu ya mpira wa miguu wa Tanzania (kipindi cha Maximo) ilikwenda kucheza na Cape verde wakiwa na Boeing ya Air Tanzania kwa wakati huo, cha ajabu wa Cape verde hawakuwahi kuona ndege kubwa kubwa kutua mjini Praia na habari zikaenea mji mzima kuwa nchi tajiri imekuja kucheza Cape verde kisa ndege hiyo ni kubwa na kwakuwa iliwasubiri wachezaji kwa siku zote walizokuwa Cape verde. Kuna mabinti wazuri sana Cape verde hawa wa kuitwa mapoint five ila usishangae amebeba sinia la ndizi akiuza mjini Praia ni kawaida sana.
13) Cape verde ni nchi inayoongoza kwa Demokrasia Africa. Hata hovyo tangu miaka ya 90 uchumi wa Cape Verde ulianza kuimarika, uchumi wao kwa sasa upo juu kuliko wa kwetu ukiangalia kwa mtu mmoja mmoja.
sisi GDP per capital ni USD 998 Wao Cape Verde ni USD 4019.8 yaani pato la mtanzania la miaka mitatu na nusu ni sawa na pato la mcape verde la mwaka mmoja tu.
12) Mnamo 2011, Rais Mstaafu wa Cape Verde Pires alitangazwa mshindi wa Tuzo ya Mo Ibrahim ya Utawala Bora kutokana na mafanikio yake katika kuleta demokrasia,uimara na neema katika kisiwa cha Cape Verde.
Pedro Verona Pires aliweka msingi wa kuwaondoa wananchi wake kutoka kwenye lindi la umasikini na pia alilikataa wazo la kuibadilisha katiba ili kumwezesha kugombea Urais tena.
0 comments:
Post a Comment