BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAWENZI MARKET FC YAHAHA KUSAKA SH4 MIL KUJIANDAA NA JKT OLJORI LIGI DARAJA LA PILI.

Juma Mtanda, Morogoro.
Viongozi wa klabu ya Mawenzi Market FC ya Morogoro wametangaza kukumbwa na ukata wa kifedha na kulazimika kuingia mtaani kuomba fedha kwa wadau wa soka ili kupata kiasi cha sh4 mil kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa mwisho dhidi ya JKT-Ojoro ya Arusha ligi daraja la pili hatua ya nne bora utaopigwa jumamosi uwanja wa jamhuri mkoani hapa.

Akizungumza na gazeti hili mjini hapa, Mlezi wa klabu hiyo, Afred Katabarura alisema kuwa ni kweli klabu yao imekumbwa na ukata wa kifedha na tayari wameanza kuomba fedha kwa wadau wa soka ili kupata fedha kiasi cha sh4 mil ikiwa ni maandalizi katika mchezo wao wa mwisho wa ligi hiyo.

Katabarura alisema kuwa mchezo kati yao na JKT-Ojoro wanaungalia kwa jicho la pili hivyo wanalazimika kufanya maandalizi ya kutosha kwa timu yao ili kupata matokeo yatayowawezesha kupata moja ya nafasi tatu za kufuzu kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao.

“Mawenzi Market FC ina pointi sita na lengo letu ni kupata ushindi katika mchezo dhidi ya JKT-Ojoro ili kumaliza na pointi tisa hivyo tunasaka fedha kiasi cha sh4 mil kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo ili tupate matokeo yatayotuwezesha kufuzu kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao.”alisema Katabarura.

Katabarura alisema kuwa fedha hizo zitatumika katika kuweka kambi, kulipa posho wachezaji, chakula na usafiri kwa ajili ya timu kwenda uwanjani katika mazoezi jioni na asubuhi ambapo kambi tayari imeanza kuwekwa.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya mipango, uchumi na fedha klabu ya Mawenzi Market FC, Joseph Chalo alisema kuwa tayari kuna watu wameteuliwa kuchangisha fedha eneo la soko la Mawenzi na mitaa ya Manispaa hiyo.

Chalo alisema kuwa licha ya klabu hiyo kuwapa kazi baadhi ya viongozi kuchangisha fedha kwa wadau mitaani, wameongeza wigo kwa wadau kuchangia fedha kupitia 0677203746 baada ya klabu hiyo kusajili namba hiyo kwa jina la klabu ya Mawenzi Market FC.

“Tunawaomba wadau wa soka ndani na nje ya Manispaa ya Morogoro kuisaidia timu kwa kuchangia fedha ili tuweze kutimiza ndoto za kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao kwani hatuwezi kupata ushindi kama timu haijafanya maandalizi ya kutosha.”alisema Chalo.

Msimu wa ligi hiyo unaonyesha kuwa JKT-Ojoro na Transit Camp zina point inane kila mmoja huku Mawenzi Market FC na Cosmo Politan FC zenye zina pointi sita zikitofautiana magoli ya kufunga na kufungwa ambapo wiki hii ligi hiyo itafikia ukingo.

Timu tatu zitafuzu moja kwa moja kuingia ligi daraja la kwanza msimu ujao huku timu moja ikibakia ligi daraja la pili.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: