BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MSANII NEY WA MITEGO AKAMATWA MOROGORO

Emanuel Elibariki maarufu Nay Wa Mitego.

Jeshi la Polisi limethibitisha kumkamata na kumshikilia rapa wa muziki wa kizazi kipya, Emanuel Elibariki maarufu Nay Wa Mitego leo usiku mjini Morogoro.

Akizungumza na Mwananchi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alithibitisha kumkamata rapa huyo kwa kosa la kutoa wimbo unaoikashifu serikali. 


“Alikamatwa saa nane usiku wa leo, kwa kosa la kutoa wimbo wenye maneno ya kashfa dhidi ya Serikali na shauri lake lipo Dar es Salaam kwa sasa, atapelekwa kuhojiwa kuhusiana na masuala yake ya kazi zake za sanaa kwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa,” alisema Kamanda Matei.Chanzo/Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: