TANZANIA YAKUBALI KUTOA MADAKTARI 500 KWENDA NCHINI KENYA
Serikali ya Tanzania imekubali ombi la Kenya la kuisaidia nchi hiyo na madaktari 500 watakaosaidia kukabiliana na tatizo la uhaba wa madaktari katika vituo vyake vya tiba kufuatia kutokea kwa mgomo wa madaktari nchini humo.
Rais wa taifa hilo John Pombe Magufuli amekubali kutoa madaktari hao baada ya kufanya mazungumzo na ujumbe wa Kenya wa maafisa wa afya uliotumwa kwake na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Kiongozi huyo amesema kuwa Tanzania imekubali ombi hilo kwa kuwa Kenya ni jirani ,ndugu na rafiki wa kweli wa Tanzania na amemtaka waziri wa afya nchini humo Ummy Mwalimu kuharakisha mchakato huo ili maafisa hao waelekee Kenya kutekeleza jukumu hilo.

''Matatizo ya Kenya ni matatizo ya Tanzania, tutawapatia madaktari hao 500 wakatoe huduma kwa ndugu zetu waliopo Kenya na kwa kuwa mumenihakikishia kuwa madaktari wangu watalipwa mishahara inavyostahili, kufanya kazi katika mazingira mazuri mbali na kuwapa nyumba za kuishi, sina tatizo naamini mambo yatakuwa mazuri'', alisema Magufuli.
Waziri wa afya wa Kenya Dkt. Cleopa Mailu ambaye aliongoza ujumbe huo alimweleza rais Magufuli kwamba baada ya mgomo wa madaktari pamoja na uamuzi wa taifa hilo kugatua madaraka katika sekta ya afya imebainika kuwa taifa hilo lina uhaba mkubwa wa madaktari ambao hauwezi kumalizwa kwa kutegemea madaktari wanaosomeshwa nchini humo bali kupata madaktari kutoka nje.
Mheshimiwa Jack Ranguma ambaye alikuwa katika ujumbe huo wa Kenya amesema kuwa Kenya itawalipa madaktari hao kwa stahili zote ikiwa ni mishahara na nyumba za kuishi.
Naye waziri wa afya na ustawi wa jamii nchini Tanzania Ummy Mwalimu amesema kuwa wizara yake iko tayari kutoa madaktari hao haraka iwezekananvyo akisema kuwa Tanzania ina madaktari wengi wazuri ambao wamehitimu lakini hawajapata ajira, huku wengine wakimaliza mikataba yao ya kazi wakiwa na uwezo wa kufanya kazi.
''Kwa hiyo nitoe wito kwa madaktari wote nchini Tanzania ambao hawapo katika utumishi wa umma, hawapo katika hospitali teule na ambao hawapo katika hospitali za mashirika yasiokuwa ya serikali wanaolipwa na serikali waombe nafasi hizi''
''Vigezo tunavyaongalia ni kwanza awe amemaliza mafunzo ya vitendo yani Internship, pili awe amesajiliwa na baraza la madaktari la Tanganyika. Kwa hiyo leo hii tunatoa tangazo na tumefurahi sana kwa sababu tuna madaktari wa kutosha ndani ya nchi na tunaweza kuwapeleka Kenya'',alisema muheshimiwa Ummy.BBC
0 comments:
Post a Comment