BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JE WAJUA KUWA DUNIA MZIMA INA MITI 60,000 LAKINI MITI ADIMU ZAIDI IPO KATIKA ARDHI YA TANZANIA


DUNIANI kunaelezwa kuna aina 60,065 za miti iliyopo, kwa mujibu wa utafiti uliofanyika, huku Tanzania ikiwa na mti sita adimu kuliko yote.

Asasi ya Botanical Gardens Conservation International (BGCI), kwa kutumia mitandao ya kitafiti 500, imefanyia kazi na kubani idadi hiyo.

Wataalamu hao wanaamini kwamba takwimu hizo zitakuwa za manufaa kwao kwa ajili ya kutambua mbegu adimu za miti na mimea na namna ya kuzihifadhi ili zisitoweke

Kwa mujibu wa taarifa kutoka jarida la kisomi la Misitu Endelevu, linaeleza kuwa miongoni mwa miti na mbegu adimu za aina ya Karomia Gigas, iiliyopatikana nchini Tanzania

Pia, Brazil kumebainika ndio nchi yenye aina nyingi ya miti, jumla yake ikiwa ni 8,715, ambayo ni sawa na asilimia 14. 5 ya miti yote.

Katika ukanda wa juu kabisa wa dunia wa Kaskazini mwa dunia, ndiko kunaelezwa kuna aina chache ya miti, kutokana na uhalisia wa hali ya hewa.

Inaelezwa pia kuna aina 300 ya miti ambayo iko katika hatua ya kutoweka, jambo linalohatarisha hata kutoweka kwake.

Katibu Mkuu wa asasi ya BGCI, Paul Smith, anasema kuwa si rahisi kutoa takwimu kwa usahihi kuhusu idadi hiyo, kutokana na upekuzi na ukusanyaji wa takwimu haujaingia kwa kina.

"Tuko katika nafasi ya kipekee, kwa sababu tuna wanachama amabao ni taasisi 500 tu," anasema na kuongeza:"Takwimu nyingi hazipatikani kwa ajili ya matumizi ya umma.”

Hata hivyo, mtaalamu mwingine wa misitu aitwaye Dk. Smith anausifu utafiti uliofanyika kwamba ni muhimu sana duniani.

"Kupata taarifa muhimu, kama vile katika nchi ipi kuna aina hii ya miti, inatoa taarifa muhimu kwa ajili ya uhifadhi.

"Hii ni ya manufaa sana kwetu, katika kutoa kipaumbele cha uhifadhi na mahali pa kufanya tathmini ya kupata hadhi kamili ya mmea," anafafanua.

Kuhusu mmea adimu uliopatikana nchini Tanzania wa aina ya Karomia gigas, ilikuwa mwaka jana, ambayo ilikuwa sita tu.

Kutokana na hilo, wamelazmika kuajiri wa sita wa kuutunza, kama namna ya kuendeleza mbegu hiyo na wamepewa jukumu la kutoa taarifa zote muhimu, ikiwemo kufutuatilia inavyotoa mbegu.

Lengo kuu ni aina ya mti huo kukuzwa na kupatikana kwa wingi katika bustani mbalimbali ili kukuza upatikanaji wake.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: