SERIKALI imesema katika kipindi cha Januari mwaka 2010 hadi Februari mwaka huu, kumekuwa na jumla ya ajali 31,928 zilizosababisha vifo vya watu 6,529, huku majeruhi wakiwa 30,661.
Kauli hiyo, ilitolewa jana bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kiwani, Abdallah Haji Ali.
Katika swali lake, mbunge huyo alitaka kujua ni watu wangapi ambao wamepoteza maisha na wangapi wamejeruhiwa na ajali za pikipiki kuanzia mwaka 2010 hadi 2017?
Akijibu swali hilo, Waziri Mwigulu alisema pikipiki za matairi mawili (bodaboda) na matairi matatu (bajaji) zilianza kutumika kubeba abiria kuanzia mwaka 2008.
“Mwaka 2010,Serikali ilipitisha kanuni na masharti ya usafirishaji wa pikipiki. Aidha katika kipindi hicho hakukuwa na utaratibu wowote wa kusimamia biashara ya waendesha pikipiki wanaobeba watu.
“Kwa kipindi cha kuanzia Januari 2010 hadi Februari mwaka mwaka huu, kumekuwa na jumla ya ajali 31,928 zilizosababisha vifo vya watu 6529 na majeruhi 30,661,”alisema Mwigulu.
Akiuliza swali la nyongeza Mbunge wa Nungwi, Yusuph Haji Hamisi aliuliza. “Tuna mkakati gani wa kupunguza hizi ajali,” alihoji.
Katika majibu yake, Mwigulu alisema elimu iendelee kutolewa kwa kila mkoa na wilaya kwa idara inayoshughulikia usafiri ili waache kuendesha bodaboda kwa mwendo kasi.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment