WAPUMBAVU WAMZUSHIA KIFO MWANASIASA MKONGWE DK MZINDAKAYA ALIYELAZWA MUHIMBILI
Mwanasiasa mkongwe na kada wa CCM, Dk Chris Mzindakaya
Dar es Salaam. Mwanasiasa mkongwe na kada wa CCM, Dk Chris Mzindakaya amesikitishwa na watu wanaovumisha taarifa kuwa amefariki na kuwaita ni wapumbavu.
Akizungumza leo akiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), Mzindakaya amesema afya imeimarika zaidi na ataruhusiwa kuondoka hospitalini hapo wakati wowote.
Usiku wa kuamkia leo mtandao ya kijamii ilikuwa ikisambaza taarifa potofu za kifo chake.
Baada ya uvumi huo,Dk Mzindakaya alitoa kauli hiyo leo huku akiwahakikishia waandishi kuwa baada ya matibabu, madaktari wamemweleza Afya yake imeimarika mfano wa kijana wa miaka 20.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment