MSANII aliyedaiwa kuchora nembo ya Taifa yenye picha ya Adam na Hawa, Francis Maige maarufu (Ngosha) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Ngosha ambaye alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipopelekwa wiki iliyopita akitokea hospitali ya Amana, amefariki dunia saa 2 usiku Mei 29.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Hospitali ya Muhimbili imeeleza kuwa hali ya Ngosha ilibadilika ghafla akiwa hospitali hapo. “Mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha maiti hapa Muhimbili na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa na mamlaka husika.” imesema taarifa hiyo.
0 comments:
Post a Comment