Hayo yalibainishwa jana Bungeni na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kaliua(CUF), Magdalena Sakaya.
Sakaya alitaka kujua ni ajali ngapi za bodaboda zimetokea kwa miaka mitatu tangu mwaka 2015 mpaka 2017 na watu wangapi wamepoteza maisha kwenye ajali hizo na walemavu ni wangapi.
Nchemba alisema ajali hizo zimesababisha majeruhi na walemavu 4,696 na kutaja mikakati ya kupitishwa kwa kanuni ya leseni za pikipiki za kubeba abiria mwaka 2009, kutoa elimu ya usalama barabarani mashulenajali hizo zimesababisha majeruhi na walemavu 4,696 na kupitia vipindi vya radio, televisheni na vipeperushi.
Alisema kati ya mikakati hiyo ni kupitishwa kwa kanuni ya leseni ya pikipiki na bajaji pamoja na kutoa elimu ya usalama barabarani mashuleni pamoja na vyombo vya habari.
0 comments:
Post a Comment